
Wenyeviti wa taasisi za kidini na kisayansi za Iran, katika barua ya pamoja kwa kiongozi mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, wamepongeza “msimamo wake wa ujasiri” na kueleza matumaini kuwa utasaidia kumaliza migogoro inayoendelea.
“Kukosoa kwako mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Iran na mauaji ya watu wasio na hatia kumezijengea heshima jumuiya za kidini duniani kote,” imesema barua hiyo iliyotumwa kwa Papa Leo XIV na kutolewa Jumamosi.
Imeongeza kuwa upinzani wa Papa dhidi ya mashinikizo ya kisiasa ya rais wa Marekani ni “mfano wa kuigwa na wanazuoni na viongozi wa dini zote.”
Waliotia saini barua hiyo wamesisitiza kuwa ujumbe wa Manabii wa Mungu umekuwa daima ni amani, mshikamano wa binadamu, kupinga dhuluma na ukatili.
Wakitoa mifano kutoka kwenye mafundisho ya kidini, wameeleza kuwa mauaji ya mtu mmoja asiye na hatia ni sawa na kuua wanadamu wote.
“Licha ya ukweli huo, utawala wa Israel umaoua watoto kwa msaada wa Marekani, umeshambulia nchi kadhaa katika miaka mitatu iliyopita na kuua makumi ya maelfu ya wanaume, wanawake na watoto wasio na hatia huko Gaza, Lebanon, Syria, Iran, Iraq, Yemen na Qatar,” imesema barua hiyo.
Imeashiria vita vya kidhalimu vya Marekani na Israel dhidi ya Iran vilivyoanza mnamo Februari 28, na kusema kuwa pande hizo mbili zilivuka mipaka yote kwa kumuua Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, na kushambulia miundombinu ya raia na maeneo umma vikiwemo vyuo vikuu, shule, na vituo vya kutoa misaada.
Waandishi wa barua hiyo wamesema kuwa rasilimali zinazotumiwa kwa ajili ya mizozo!kama hiyo zinapaswa kutumiwa kukuza maadili mema na kupunguza mateso ya binadamu.Maoni hayo yanafuatia kauli za awali za Papa Leo, ambaye alionya kuhusu kuongezeka ghasia na ukosefu wa amani katika eneo la Asia Magharibi.
“Utulivu na amani havitengenezwi kwa vitisho au silaha,” alisema Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, akihimiza kuwepo “mazungumzo yenye busara, halisi na kuwajibika.”
Pia alionya kuwa kuongezeka ghasia na machafuko kunaweza kusababisha mgogoro mkubwa kwa binadamu.