#HABARI: Kamandi Kuu ya Jeshi la Iran hapo jana ilitangaza kuwa itarejesha vizuizi vyote kwenye Mlango Bahari wa Hormuz, hatua inayobadili msimamo wake iliyouchukua juzi Ijumaa wa kuufungua mlango huo muhimu wa bahari.
Juzi Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Iran Abbas Araghchi alitangaza kufunguliwa kikamilifu wa Mlango Bahari wa Hormuz kama sehemu mazungumzo yake na Marekani.
Tehran iliifunga njia hiyo nyembamba ya bahari inayopitisha karibu asilimia 20 ya mafuta na gesi yote asili duniani baada ya Marekani na Israel kuishambulia dola hiyo ya Uajemi mwishoni mwa mwezi Februari.
Hii leo, taarifa iliyotolewa na Kamandi Kuu ya Jeshi la nchi hiyo imesema Washington imekiuka ahadi ya kufungua kikamilifu shughuli zote za usafirishaji kupitia mlango habari huo kwa uamuzi wake wa kuendelea na mzingiro wa kijeshi iliyouweka mwanzoni mwa wiki hii.
Rais Donald Trump wa Marekani aliamuru jeshi la nchi hiyo kuweka vizuizi kwa shughuli zote za bandari za Iran ikiwa ni pamoja na kuzuia kuingia na kutoka kwa meli zinazobeba shehena ya mafuta ya Iran.
Iran imesema hadi pale Marekani itakapoondoa mzingiro kwa meli zinazoelekea kwenye dola hiyo ya kiislamu, “hali kwenye Mlango Bahari wa Hormuz itasalia chini ya usimamizi mkali” wa Tehran.

(Feed generated with FetchRSS)