Rais Samia Suluhu Hassan, amesema shughuli za baba lishe na mama lishe zina hadhi na zinapaswa kuheshimiwa kutokana na mchango wake katika afya na ustawi wa jamii.

Rais Samia amesema hayo Aprili 21, 2026 jijini Dar es Salaam wakati wa kongamano la kwanza la baba lishe na mama lishe.

Amesisitiza kuwa kundi hilo halipaswi kunyanyaswa wala kubaguliwa, kwani linachangia kwa kiasi kikubwa upatikanaji wa chakula na huduma muhimu kwa wananchi.

Ameongeza kuwa ni muhimu kutambua na kulinda shughuli hizo kama sehemu ya mfumo wa uchumi na ustawi wa jamii.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *