Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa TOSCI, Zubery Suddy, amesema ubora wa mbegu unasimamiwa kwa kuzingatia taratibu na viwango vya kisheria vinavyohusisha hatua mbalimbali za ukaguzi.

Ameeleza kuwa mchakato huo unajumuisha ukaguzi wa mashamba ili kufuatilia namna shughuli za kilimo zinavyoendeshwa, pamoja na upimaji wa mbegu ili kubaini kama zinakidhi vigezo vinavyotakiwa kwa matumizi ya kilimo. Aidha, tathmini hufanyika ili kuhakikisha mbegu zina uwezo na ufanisi unaolingana na mazingira ya eneo husika.

#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *