
Wakati wa ziara ya Gustavo Petro huko Caracas, rais wa Colombia na rais wa mpito wa Venezuela wametangaza siku ya Ijumaa, Aprili 24, ushirikiano kati ya vikosi vyao vya kijeshi na idara za kijasusi kando ya kilomita 2,000 za mpaka wanaoshiriki. Lengo: “kuyaandgamiza makundi ya mafia na magenge ya wahalifu katika eneo hilo.”
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kiongozi wa kwanza wa kigeni kuzuru Venezuela tangu kutekwa nyara kwa Nicolas Maduro na Marekani mnamo Januari 3, Rais wa Colombia Gustavo Petro, kiongozi wa mrengo wa kushoto anayeshirikiana na rais wa zamani wa Venezuela na Venezuela yenyewe, alipokelewa katika ikulu ya Miraflores huko Caracas na Delcy Rodríguez, rais wa mpito wa Venezuela, siku ya Ijumaa, Aprili 24.
Ajenda ya mkutano kati ya washirika hao wawili ilijumuisha, haswa, suala la ushirikiano wao wa kibiashara na nishati—hasa usafirishaji wa gesi hadi Colombia—pamoja na usalama kando ya mpaka wa zaidi ya kilomita 2,000 kati ya nchi zao mbili.
Baada ya mkutano huo, Gustavo Petro na Delcy Rodriguez walijadili ushirikiano kati ya vikosi vyao vya kijeshi na idara za kijasusi ili “kuvunja makundi ya mafia na magenge ya wahalifu katika eneo hilo,” anaripoti mwandishi wetu huko Caracas, Alice Campaignolle.
Wakati makundi ya kijeshi yakiongezeka katika eneo hili hatari sana, Caracas na Bogotá “zitatekeleza juhudi za pamoja na zilizoratibiwa kwa kina ili kuzikomboa jamii za mpakani kutoka kwa makundi ya mafia yanaojihusisha na shughuli mbalimbali haramu, kuanzia na kokeni, dhahabu haramu, biashara haramu ya binadamu, na madini adimu,” alisema Gustavo Petro.
“Nchi zetu mbili zimejitolea kuendeleza […] mipango ya kijeshi, lakini pia kuanzisha mara moja mifumo ya kushiriki taarifa na maendeleo ya kijasusi,” alitangaza Delcy Rodriguez, akibainisha kwamba Colombia na Venezuela zinashiriki “mbinu nzito sana na pana sana ya jinsi mapambano dhidi ya magenge ya wahalifu yanavyopaswa kuwa.”
Lakini zaidi ya matangazo haya, ziara ya rais wa Colombia huko Caracas pia inawakilisha hatua ya mabadiliko katika Venezuela baada ya Maduro. Kufuatia shambulio la Marekani la Januari 3, inaweza kutafsiriwa kama aina ya kuanzisha uhusiano na rais Delcy Rodriguez, ambaye hadi sasa, hajatangaza kufanyika hivi karibuni kwa uchaguzi, kama inavyoainishwa na Katiba ya nchi katika tukio la kutokuepo kwa kiongozi wa nchi.
Wakati Donald Trump akielezea kuridhika kwake na ushirikiano wa kiongozi huyo zaidi ya miezi mitatu baada ya kuchukua hatamu za madaraka chini ya uangalizi wa Washington, je, tunapaswa kuhitimisha kwamba matarajio ya mabadiliko ya kisiasa yanayowezekana yanafifia nchini Venezuela?