Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi na wengine huko Gaza wameanza kupiga kura leo Jumamosi, Aprili 25, kuwachagua mameya wao. Kwa jumla, karibu watu milioni 1.5 wamejiandikisha kupiga kura katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wapalestina katika Ukingo wa Magharibi na wengine huko Gaza wameanza kupiga kura Jumamosi kuwachagua mameya na madiwani wao wa manispaa, uchaguzi wa kwanza tangu kuanza kwa vita vya Gaza, katikati ya kuchanganyikiwa na chaguzi chache.

Karibu watu milioni 1.5 wamejiandikisha kupiga kura katika Ukingo wa Magharibi unaokaliwa, na 70,000 katika eneo la Deir el-Balah (katikati mwa Ukanda wa Gaza), maeneo mawili husika, kulingana na Tume kuu ya Uchaguzi, yenye makao yake makuu Ramallah.

Hakuna orodha za viongozi wa Hamas

Wakati wa ufunguzi wa vituo vya kupigia kura saa 1:00 asubuhi (12:00 Afrka ya Kati), picha za AFP zilizopigwa Al-Bireh, katika Ukingo wa Magharibi, na Deir el-Balah zimeonyesha maafisa wa uchaguzi katika vituo vya kupigia kura, huku Wapalestina wachache wakijitokeza kupiga kura. Orodha nyingi za wagombea ni kutoka Fatah, chama kisicho cha kidini cha Rais wa Palestina Mahmoud Abbas, au wagombea binafsi.

Hata hivyo, hakuna orodha inayodai kuwa na uhusiano na Hamas, chama pinzani cha Fatah, ambacho kinadhibiti karibu nusu ya Ukanda wa Gaza na ambacho shambulio lake la Oktoba 7, 2023 dhidi ya Israel lilisababisha vita.

Mahmoud Bader, mfanyabiashara kutoka Tulkarem, kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi, anasema atapiga kura, lakini bila udanganyifu wowote. 

“Wagombea huru au kutoka chama chochote, hawatabadilisha chochote katika jiji hili,” ameliambia shirika la habari la AFP, akibainisha kuwa Israel imedhibiti kambi mbili za wakimbizi jirani kwa zaidi ya mwaka mmoja. “Ni uvamizi (wa Israel) unaoendesha Tulkarm,” ameongeza.

Katika miji mingine mikubwa, ikiwa ni pamoja na Nablus na Ramallah, mgombea mmoja tu ndio yuko kwenye orodha. Vituo vya kupigia kura vitabaki wazi hadi saa 1:00 usiku (12:00 jioni saa za Afrika ya Kati) katika Ukingo wa Magharibi, wakati Deir el-Balah, vitafungwa saa 11:00 jioni  saa za Afrika ya Kati ili zoezi la uhesabuji kura lifanyike mchana, kutokana na ukosefu wa umeme.

“Fursa muhimu”

Naibu Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa wa Mchakato wa Amani wa Mashariki ya Kati, Ramiz Alakbarov, amekaribisha hatu hii ya kufanyika kwa uchaguzi huu na akasema kwamba “ni fursa muhimu kwa Wapalestina kutekeleza haki zao za kidemokrasia katika wakati mgumu sana.”

Huko Gaza, eneo linalodhibitiwa na Hamas tangu mwaka 2007, huu ni uchaguzi wa kwanza tangu uchaguzi wa wabunge wa 2006, ambao kundi hilo lilishinda.

Kulingana na mtaalamu wa masula ya siasa Jamal al-Fadi wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar huko Cairo, Mamlaka ya Palestina inafanya uchaguzi huko Deir al-Balah, Gaza pekee, “kama jaribio (la kutathmini) mafanikio au kushindwa kwake, kwani hakukuwa na kura za maoni” tangu kusitisha mapigano mwezi Oktoba 2025.

Pia ni mojawapo ya maeneo machache katika eneo hilo, yaliyoharibiwa na miaka miwili ya mashambulizi ya anga ya Israel, ambapo raia hawajahama kwa wingi kutokana na vita. Bw. Abbas, mwenye umri wa miaka 90, amesalia madarakani tangu kuchaguliwa kwake mapema mwaka 2005, na ahadi zake za kuandaa uchaguzi wa rais na wabunge hazikutimizwa kamwe.

Farah Chaath, mkazi wa Deir al-Balah, amesema ana furaha kupiga kura kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 25, akiongeza kuwa uchaguzi huo “ni uthibitisho wa kuendelea kwetu kuwapo katika Ukanda wa Gaza hata kama.”

Tume ya uchaguzi imesema imeajiri “kampuni ya usalama ya kibinafsi ili kulinda vituo vya kupigia kura” huko Gaza, msemaji wake, Farid Taamallah, ameliambia shirika la habari la AFP.

Lakini chanzo ndani ya tume hiyo huko Gaza, ambacho kimeomba kutotajwa jina, kimesema kwamba “polisi wa Hamas wamebainisha kuwa watalinda usalama wa mchakato wa uchaguzi huko Deir al-Balah,” wakimaanisha kupelekwa kwa “walinda usalama wasio na silaha wakiwa wamevaa nguo za kawaida” kuzunguka vituo vya kupigia kura.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *