Wajumbe kutoka Marekani wanatarajiwa jijini Islamabad nchini Pakistan siku ya Jumamosi, kwa ajili ya mazungumzo ya amani ya awamu ya pili na wawakilishi wa Iran.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt, amesema Makamu wa rais JD Vance hatokwenda kwa sasa lakini Steve Witkoff na Jared Kushner wapo njiani kwenda Islamabad.

Hata hivyo, Shirika la Habari la serikali nchini Iran linasema, wawakilishi wa Tehran hawana mpango wa kukutana na wenzao wa Marekani kwenye mazungumzo ya ana kwa ana.

Tayari kiongozi wa ujumbe wa Iran, wakiongozwa na Waziri wake wa Mambo ya nje Abbas Araghchi, aliwasili jijini Islamabad siku ya Ijumaa, na tayari amekutana na kufanya mazungumzo na mkuu wa majeshi wa Pakistan Field Marshal Asim Munir.

Kuelekea mazungumzo hayo, suala la kufungua eneo la mlango wa Bahari wa Hormuz, linasalia suala tata na gumu kati ya Marekani na Iran.

Rais Donald Trump, ameendelea kusisitiza kuwa Marekani itazuia meli za Iran na bandari zake hadi Tehran itakapokubali mkataba wa amani na kuachana kabisa na mradi wake wa nyuklia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *