#HABARI: Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amewataka wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mnazi Mmoja kusoma kwa bidii na kuzingatia masomo yao ili kuongeza kiwango cha ufaulu shuleni hapo.
Mpogolo ametoa kauli hiyo, wakati alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa madarasa 20 yenye jumla ya matundu 45 katika shule hiyo, mradi unaotekelezwa kwa gharama ya Shilingi Bilioni 1.8, na kusema kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa iliyokuwepo kwa muda mrefu na kuwawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora zaidi.
Ameeleza kuwa tangu mwaka 2007 shule hiyo ilikuwa ikikabiliwa na changamoto ya miundombinu, hali iliyosababisha wanafunzi kutumia vyumba vikubwa visivyokidhi mahitaji.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Dkt. Mussa Ally, amesema ujenzi wa madarasa hayo utaongeza ufanisi wa utoaji elimu na kusaidia wanafunzi kupata elimu bora.
Amesema Halmashauri itaendelea kutekeleza miradi ya maendeleo katika sekta ya elimu ili kuhakikisha changamoto za miundombinu zinapungua na wanafunzi wanapata fursa sawa za kujifunza.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.
(Feed generated with FetchRSS)