Polisi nchini Marekani wamesema bado wanachunguza chanzo cha tukio la mtu anayetuhumiwa kufyatua risasi wakati wa hafla ya chakula cha jioni ya waandishi wa habari wa Ikulu iliyokuwa ikifanyika katika hoteli ya Washington Hilton na kuhudhuriwa na Rais wa Marekani Donald Trump.
Mamlaka za Marekani zimemtaja mtuhumiwa wa tukio hilo kuwa ni Cole Tomas Allen, mwenye umri wa miaka 31 kutoka California na anatarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu kujibu mashtaka yake.
Kwenye mkasa huo, Trump na mkewe Melania waliondolewa haraka kutoka kwenye hafla hiyo na maafisa wa Idara ya Usalama baada ya mwanaume huyo kumfyatulia risasi afisa wa kitengo cha ulinzi wa rais kabla ya kukabiliwa na kukamatwa.
Mhariri | @rajjmsangi
#AzamTvUpdates
(Feed generated with FetchRSS)