Lindi. Mwenge wa uhuru umepokelewa leo kutoka mkoani Pwani na unatarajiwa kukimbizwa mkoani humo km 920, miradi 38 yenye thamani ya Sh15bilioni.
Akipokea Mwenge wa uhuru leo Jumatatu Aprili 27, 2026 Mkuu wa mkoa wa Lindi Zainab Telack amesema kuwa miradi hiyo yenye thamani ya Sh15bilioni itaonwa,kuzinduliwa na kuwekwa mawe ya msingi.
“Mwenge wa uhuru kwa mkoa wa Lindi utakimbizwa km 920 kwenye miradi 38, ambayo 19 itawekwa mawe ya msingi na 19 kuzinduliwa “amesema Telack.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mohamed Nyundo amesema kuwa Wilaya ya kilwa inajumla ya miradi saba miradi mitatu itawekwa mawe ya msingi na miradi minne ya maendeleo itazinduliwa ambayo miradi hiyo inathamani ya Sh400milioni.
Kwa upande wake Mkimbiza mwenge wa Uhuru Kitaifa Wazo Wang’onda ametoa ujumbe wa mwenge wa uhuru kwa wananchi wa Wilaya hiyo huku akiwahimiza kupiga vita madawa ya kulevya pamoja na mapambano dhidi ya