.

Chanzo cha picha, Reuters

Meli kubwa inayohusishwa na mmoja wa washirika wakuu wa Rais wa Urusi Vladimir Putin imepitia Mlango-Bahari wa Hormuz, licha ya njia hiyo muhimu ya baharini kufungwa.

Meli ya kifahari ya Nord, yenye urefu wa mita 142, inayohusishwa na bilionea wa Urusi Alexey Mordashov, ilisafiri kutoka Dubai hadi Muscat, Oman mwishoni mwa juma, mojawapo ya meli kadhaa za kibinafsi zilizovuka bahari hiyo katika miezi ya hivi karibuni.

Iran imeshirikiana na Urusi katika mazungumzo ya ngazi ya juu wiki hii huku mzozo kati yake na Marekani kuhusu kufunguliwa tena kwa mlango huo wa bahari ukiendelea.

Takriban moja ya tano ya usambazaji wa mafuta ghafi na gesi asilia (LNG) husafirishwa kupitia njia ya majini.

Mordashov, ambaye ana uhusiano wa karibu na Putin, hajaorodheshwa kama mmiliki rasmi wa meli hiyo ya kifahari. Lakini, rekodi za Nord zinaonyesha kuwa ilisajiliwa kwa kampuni inayomilikiwa na mkewe mnamo 2022.

Nord, anayekadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola milioni 500, aliondoka Dubai Ijumaa usiku na kufika Al Mouj, marina katika mji mkuu wa Oman, Jumapili asubuhi, kulingana na data za jukwaa la Marine Traffic.

Usafiri wa baharini kupitia mkondo wa Ghuba kwa sasa iko katika sehemu ndogo ukilinganisha na viwango vya kabla ya vita.

Mzozo huo umechangia kupanda kwa kasi kwa bei ya mafuta duniani, huku kiwango cha kimataifa cha mafuta ghafi ya Brent kikipanda hadi dola 109 za Kimarekani kwa pipa siku ya Jumatatu.

Pia unaweza kusoma:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *