#HABARI: Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imezindua mabasi matatu mapya ya watumishi yaliyogharimu zaidi ya shilingi milioni 500 kwa lengo la kuboresha mazingira ya kazi na kuongeza ufanisi.

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Daniel Mushi, ameeleza kuwa usafiri huo ni nguzo muhimu katika utekelezaji wa maono ya Serikali ya “Kazi na Utu,” kwani utasaidia kuweka mazingira wezeshi na ya kuvutia kwa watumishi wanapopambana kufikia malengo ya wizara.

Ununuzi huo umefanyika kupitia ushirikiano na mradi wa BOOST ili kurahisisha safari za kila siku za ofisini na ziara za kikazi jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu, Dkt. Edith Rwiza, amebainisha kuwa kabla ya hatua hii, watumishi walikuwa wakitumia hadi shilingi 15,000 kwa siku kwa ajili ya usafiri, hali iliyokuwa ikishusha morali ya kazi na kuleta ugumu wa maisha kwa wafanyakazi hao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa TUGHE, Bw. Moshi Kisinga, ameishukuru wizara kwa niaba ya watumishi akisema kuwa magari hayo ni suluhisho la changamoto ya muda mrefu ya usafiri.

Kufuatia hatua hiyo ya kihistoria, viongozi wametoa rai kwa watumishi kuyatunza mabasi hayo kwa weledi huku wakihimizwa kuongeza juhudi, maarifa, na uwajibikaji katika kutimiza majukumu yao ya kila siku kwa taifa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *