Naibu Waziri wa Vita wa Marekani amekiri kuwa mifumo ya makombora ya nchi hiyo haiwezi kudhamini kiwango cha kutosha cha ulinzi.

Mark Berkowitz, Naibu Waziri wa Vita wa Marekani anayeshughulikia sera za anga, amesema katika hotuba yake kwamba: Jeshi la Marekani kwa sasa halina vifaa vinavyohitajika vya kujilinda dhidi ya silaha za kasi ya juu sana na makombora ya kisasa ya cruise.

Sambamba na hayo, Jennifer Kavanagh, mkurugenzi wa uchambuzi wa kijeshi katika kituo cha tafiti za kipaumbele cha kijeshi cha Marekani, ameandika katika uchambuzi wake wa jarida la Foreign Policy kwamba: Zama za udhibiti usio na changamoto wa Jeshi la Wanamaji la Marekani zimefikia mwisho; Iran kwa kufunga Mlango Bahari wa Hormuz imeonyesha kwa urahisi kwamba Marekani haiwezi tena kusimamia “uhuru wa usafirishaji wa meli”.

Ameongeza kuwa: Kwa kutumia ndege zisizo na rubani, mabomu ya baharini na makombora ya bei nafuu, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeonyesha kuwa hakuna njia mbadala ya baharini katika Mlango Bahari wa Hormuz.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *