
Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International, limewashtumu maafisa wa usalama nchini Uganda kwa kuwauwa watu 16 kwa kuwapiga risasi huku mamia ya wafuasi wa upinzani wakikamatwa na kuteswa, wakati na baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi Januari.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ripoti ya Amnesty International, iliyotoleweka wiki hii, imesema licha ya mauaji hayo, hakuna afisa yeyote wa usalama, aliyewahi kukamatwa miezi mitatu baada ya uchaguzi huo.
Shirika hilo la kutetea haki za binadamu, linatoa wito kwa serikali ya Uganda kuwachuguza matukio hayo yaliyofanywa dhidi ya wanasiasa wa upinzani na wafuasi wao.
Wanasiasa na wafuasi wa chama kikuu cha upinzani cha NUP kinachongozwa na Robert Kyagulanyi marfi kama Bobi Wine, kama waliolengwa na maafisa wa usalama wa Uganda.
Kati ya Januarii tarehe tano jadi Machi tarehe 21, Amnesty Interntaional ilizungumza na familia na waathiriwa ambao wapendwa wao waliouliwa na kujeruhiwa.
Uganda haijazungimzia ripoti licha ya shinikizo za kutaka kuchunguza tuhma dhidi ya maafisa wa usalama, ambao Amnesty International inataka waliohusika kuchunguliwa hatua.