Saudi Arabia, Urusi na mataifa mengine 5 ya muungano wa wazalishaji mafuta duniani, OPEC, wameongeza uzalishaji katika hatua inayotarajiwa kuweka muendelezo wa upatikanaji wa bidhaa hiyo hasa baada ya kujiondoa ghafla kwa nchi ya Falme za Kiarabu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Nchi 7 ambazo ni wazalishaji wakubwa wa mafuta, sasa watazalisha mapipa laki 1 na elfu 88 kwa siku, ili kuhakikisha ugavi wa nishati hiyo unakuwa endelevu, uamuzi wanaochukua kutokana na mzozo wa eneo la mashariki ya kati uliopekelekea njia ya mlango Bahari wa Hormuzi kufungwa, kulingana na taarifa iliyochapishwa na OPEC.

Tangazo hili lilifuatia kikao cha mtandaoni cha nchi za Algeria, Iraq, Kazakhstan, Kuwait, Oman, Urusi na Saudi Arabia, ambapo hawakuitaja nchi ya Falme za Kiarabu, ambayo siku ya Ijumaa ilitangaza kujitoa kwenye muungano huo.

Wataalamu wa masuala ya uchumi wanasema ukimya wa Jumuiya hiyo kuhusu kujitoa kwa nchi ya Falme za Kiarabu kunaashiria kuwa kuna mvutano kwenye uhusiano wao hasa baada ya hivi karibuni, Iran kushambulia nchi Jirani zinazoshirikiana na Marekani.

Aidha wataalamu hawa wamesema kuongezwa kwa mapipa zaidi ya laki 1 kwenye idadi ya sasa ya mapipa ghafi, kutasaidia kupunguza upungufu ambao ungeweza kushuhudiwa baada ya Falme za Kiarabu kujitoa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *