
Mashirika matatu makubwa ya afya duniani katika taarifa yao ya pamoja yamelaani kushindwa kwa jumuiya ya kimataifa kuwalinda wafanyakazi wa afya, hospitali na wagonjwa katika maeneo yenye migogoro.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na WHO, ICRC na MSF wahudumu wa afya wameuawa na wengine kujeruhiwa wakati miundombinu ya afya ikiharibiwa vibaya katika mashambulio ya yanayotekelezwa na makundi yenye silaha au wanajeshi wa Serikali, nchi ya Sudan, Gaza na Ukraine zikitajwa kuathirika zaidi.
Kuhusu Sudan, ICRC imeonya kuwa kuendelea kulenga miundombinu ya afya na mashambulio dhidi ya wahudumu wa afya ni tishio kubwa kwa raia wa haswa wakati huu baadhi ya maeneo yakiripoti baa la njaa.
ICRC vilevile imeonya kuwa watoto wanaendelea kukabiliwa na visa vya utapia mlo kutokana na ukosefu wa lishe bora na matibabu muhimu kwao baada ya vituo vya afya kuharibiwa kwenye mashambulio na baadhi kufungwa.
Taarifa yao imetolewa ikiwa ni miaka 10 baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupitisha kwa kauli moja Azimio nambari 2286 linalolaani mashambulizi dhidi ya vituo vya afya, wafanyakazi wa afya na wagonjwa.