Marekani inasubiri jibu kutoka kwa Iran, kuhusu mapendekezo ya kusitisha vita katika eneo la Mashariki ya Kati, na kufunguliwa tena kwa mlango wa Bahari wa Hormuz, ili kuruhusu safari za meli za mizigo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais Donald Trump amesema ana matumaini kuwa suluhu itapatikana hivi karibuni, wakati huu Iran ikisema itapitia mapendekezo hayo 14  kabla ya kutoa jibu kwa Pakistan ambayo ni mpatanishi wa mzozo huo.

Makubaliano yoyote, yataendelea kuongeza muda wa usitishwaji vita ambao umekuwa ukiendelea na kutuliza hali nchini Lebanon, ambayo mkataba wake wa kusitisha vita na Israeli sio thabiti.

Wakati Marekani ikisubitri ripoti kutoka kwa Iran, Irael nayo imeendelea kurusha makombora Lebanon.
Wakati Marekani ikisubitri ripoti kutoka kwa Iran, Irael nayo imeendelea kurusha makombora Lebanon. AP – Bilal Hussein

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje nchini Iran, Esmaeil Baqaei, amesema, Tehran itawasilisha tu maoni yake, baada ya kupitia mapendekezo hayo kwa makini.

Wiki hii kumekuwa na ripoti kuwa, mataifa hayo mawili, yanaelekea kupata mkataba wa kusitisha vita lakini pia kuelewana kuhusu hatima ya mradi wa nyuklia wa Iran, ambao Marekani imesisitiza kuwa ni lazima Tehran iachana kabisa na mradi huo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *