
Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amewasihi wananchi wake siku ya Jumapili kupunguza matumizi yao ya petroli na mafuta ya dizeli kutokana na usumbufu wa usambazaji unaosababishwa na vita katika Mashariki ya Kati.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Tunahitaji kupunguza matumizi yetu ya petroli na dizeli. Katika miji kunapatikana usafiri wa treni za mwendo kasi, tunapaswa kujaribu kutumia vyombo hivyo… Ikiwa ni lazima tutumie gari, tunapaswa kujaribu usafiri wa umma,” amesema katika mkutano katika jimbo la kusini la Telangana.
Modi ameongeza kuwa kupunguza matumizi ya jumla ya mafuta pia ni muhimu ili kuokoa fedha za kigeni zinazotumika kwa uagizaji. “Lazima pia tuzingatie sana kuhifadhi fedha za kigeni, kwani petroli na dizeli zimekuwa ghali sana duniani kote,” amesema.
Waziri Mkuu wa India pia amewasihi raia wake kuanza tena programu za kuokoa nishati zilizotekelezwa wakati wa mlipuko wa UVIKO-19. “Lazima tuweke kipaumbele tena kwa kazi tukiwa nyumbani, mikutano ya mtandaoni na kadhalika,” ameshauri.