Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesebaini siku ya Jumapili kwamba nchi yake “haijawahi kufikiria” “kutuma” jeshi la majini katika Mlango-Bahari wa Hormuz, bali ujumbe wa usalama “kwa kushauriana na Iran.”

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amesema kuwa nchi yake “haijawahi kufikiria” “kutuma” jeshi la majini katika Mlango-Bahari wa Hormuz, bali ujumbe wa usalama “kwa kushauriana na Iran.” Alikuwa akijibu Iran, ambayo ilitishia “jibu lenye maamuezi na la haraka” iwapo Ufaransa na Uingereza zitatuma majehi yao katika Mlango-Bahari wa Hormuz, kufuatia tangazo la Paris na London la kutuma meli za kivita katika eneo hilo. Hakujawahi kuwa na swali lolote la kutumwa kwa jeshi letu katik Mlango Bahari wa Hormuz, lakini tuko tayari,” Emmanuel Macron amebainisha.

Katika mkutano na waandishi wa habari jijini Nairobi, rais wa Ufaransa amebainisha kwamba alikuwa akishikilia “msimamo huu,” ambao ni kupinga “kizuizi chochote, bila kujali asili yake,” iwe kutoka Marekani au Iran, na “kukataa ushuru wowote, bila kujali asili yake,” ili “kuwezesha uhuru wa urambazaji.”

“Tumeanzisha ujumbe wa dharura, unaoongozwa na Uingereza, ambao umekusanya nchi 50 na mashirika ya kimataifa ili kuhakikisha, kwa kushirikiana na Iran na kwa kupunguza mgogoro na nchi zote za eneo hilo na Marekani, kuanza tena kwa usafiri wa baharini haraka iwezekanavyo,” hasa kwa ajili ya kusafirisha mbolea, chakula, na hidrokaboni, ameelezea.

Katika siku ya pili ya ziara yake barani Afrika, rais wa Ufaransa amebainiha kwamba “bara zima la Afrika kwa sasa linakabiliwa na vikwazo” vya Mlango-Bahari wa Hormuz, ambapo sehemu kubwa ya mafuta yanayosafirishwa kutoka Mashariki ya Kati hupitia kwa kawaida.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *