Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa hakusafiri kwenda Nairobi kwa ajili ya mkutano wa kiuchumi kati ya Ufaransa na Afrika. Badala yake, amehutubia taifa jioni ya Jumatatu, Mei 11, ili kujibu taharuki ya kisiasa na kisheria. Kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Katiba wiki iliyopita wa kubatilisha uchaguzi wa kura ya Bunge ya mwaka 2022, mkuu wa nchi anaweza kukabiliwa na kesi za kutimuliwa malakani. Sababu: mwenendo wake wakati wa wizi katika shamba lake la “Phala-Phala” mwaka wa 2020.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Johannesburg, Claire Bargelès

Kulingana na ripoti ya mwaka 2022 ya jopo huru lililotumwa na Bunge, kuna ushahidi unaobainisha kwamba Cyril Ramaphosa alifanya utovu mkubwa wa nidhamu na kukiuka Katiba kwa kujaribu kuficha wizi wa pesa zilizofichwa kwenye shamba lake.

Wabunge wa Afrika Kusini wakati huo—zaidi ya nusu yao wakiwa wanachama wa ANC—walikataa matokeo haya katika kura ambayo sasa imebatilishwa na mahakama.

Kwa hivyo, Mahakama ya Katiba imemlazimisha Spika wa Bunge kuwasilisha ripoti hiyo kwa kamati ya kumshtaki, lakini kwa kiongozi huyo wa Afrika Kusini, licha ya uvumi wa kutimuliwa kwake, hakuna haja, kwa sasa, ya kujiuzulu.

“Sitajiuzulu”

“Nataka kusema kwa heshima kwamba sitajiuzulu. Kujiuzulu kunamaanisha kupuuza mchakato ulioainishwa na Katiba, kutoa uaminifu kwa ripoti ambayo kwa bahati mbaya imejaa makosa, na kukwepa jukumu nililokubali nilipokuwa Rais wa Jamhuri,” alitangaza Cyril Ramaphosa.

Badala ya kujiuzulu, Cyril Ramaphosa anatumia haki yake ya kuomba mapitio ya kimahakama ya ripoti hiyo inayomhusisha,

“mbinu za kupata muda,” kulingana na chama cha EFF chenye msimamo mkali wa mrengo wa kushoto, ambacho kimeazimia kuendelea kuweka shinikizo kwa mkuu wa nchi.

Chama cha ANC hakijapata wingi kamili katika Bunge la taifa tangu mwaka 2024, lakini ikiwa kura ya kumtimua mamlakani itapigwa, itahitaji theluthi mbili ya wabunge kupitisha.

Kulingana na vyombo vya habari vya ndani, ANC imeitisha uongozi wake kwa mkutano wa dharura leo Jumanne jioni, Mei 12, huko Cape Town.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *