
Mkutano wa Africa Forward unaendelea leo jijini Nairobi. Siku ya Jumatatu, Mei 11, ulilenga uchumi kwa jukwaa la biashara linalowakutanisha viongozi wa biashara kutoka Ufaransa na kote Afrika. Leo Jumanne, Mei 12, 2026, mkutano huu wa uchumi kati ya Ufaransa na Afrika utagubikwa zaidi na masuala ya kisiasa, huku wakuu wa nchi na serikali 32 wakitarajiwa katika mji mkuu wa Kenya.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Miongoni mwao, marais wa nchi 28 wanatarajiwa kuhudhuria mkutano huu, kulingana na Ikulu ya Élysée, anaripoti mwandishi wetu huko Nairobi, Albane Thirouard. Nchi zingine zitawakilishwa na wakuu wao wa serikali au makamu wa rais. Hata hivyo marais wa tatu wa nchi za ESA (Mali, Burkina Faso, na Niger), nchi tatu ambazo zilivunja ghafla uhusiano na Paris, hawatashiriki mkutano huo. Licha ya kutokuwepo kwa viongozi hao watatu, “nchi za Afrika Magharibi zitawakilishwa katika mkutano huo,” alitangaza Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron muda mfupi kabla ya mkutano huo mnamo Mei 10. Hivyo, viongozi wa Senegal, Côte d’Ivoire, na Togo wanatarajiwa.
Kutafuta uwekezaji
Kwa wale wanaohudhuria mkutano huo jijini Nairobi, mada kadhaa ziko kwenye ajenda. Kwanza, kutakuwa na mkutano kati ya wawakilishi wa kisiasa na takriban Wakurugenzi wakuu zaidi ya thelathini kutoka Ufaransa na Afrika kujadili viwanda na mpito wa nishati. Sekta binafsi ilijadiliwa katika mkutano huu. Rais wa Kenya William Ruto alitangaza siku moja kabla ya ufunguzi wake kwamba hakuwa akitafuta “misaada au mikopo” bali “uwekezaji.”
Ikulu ya Élysée inataka majadiliano ya wazi, ya moja kwa moja, na shirikishi na viongozi hawa wa makampuni makubwa yanayoendesha shughuli zao barani Afrika, kama vile CMA CGM, Orange, Benki ya Equity ya Kenya, na TotalEnergies, anaripoti mwandishi wetu maalum huko Nairobi, Alexis Bédu. Makampuni haya yanawakilisha zaidi ya euro bilioni 100 katika mapato barani Afrika, makumi ya mabilioni ya euro katika uwekezaji wa kila mwaka, na karibu ajira milioni moja. Viongozi wao wanatoa wito wa utulivu mkubwa na sheria ambazo hazibadiliki kila mara, hasa kuhusu kodi.
“Suluhisho zinajulikana”
Katika madai yao, wanatetea taratibu za haraka na, zaidi ya yote, mifumo mipya ya kuchangia hasara. Wanaona badhi ya dhamana kuwa muhimu kwa kuongeza uwekezaji wao barani Afrika. “Utambuzi unashirikiwa. Suluhisho zinajulikana,” wanaandika idadi kubwa ya Wakurugenzi Wakuu hawa katika makala ya maoni iliyochapishwa katika Gazeti la Le Figaro. Mazingira ya biashara barani Afrika yatakuwa mada muhimu. Kwa viwango vya juu vya riba vinavyoendelea kuzuia uwekezaji, kuna ukosefu wa fedha, hasa katika miundombinu. Leo Jumanne, muungano huu wa viongozi hawa wa makampuni utakuwa na fursa ya kuwaomba moja kwa moja wakuu wa nchi mazingira yanayoweza kutabirika na yasiyo hatari sana.
Mada nyingine muhimu katikati ya majadiliano ni usanifu wa kifedha wa kimataifa. Mageuzi yake ni mradi unaoungwa mkono na marais wa Ufaransa na Kenya. Unalenga kufanya mfumo wa kifedha wa kimataifa uwe wa usawa zaidi na uliorekebishwa vyema kulingana na mahitaji ya maendeleo ya nchi za Kusini mwa Dunia. Hatimaye, masuala ya amani na usalama katika bara la Afrika pia yatajadiliwa.