Ghana imetangaza kuwa itawarudisha raia wake 300-wanaoishi nchini Afrika Kusini, kufuatia ongezeko la visa vya wageni kushambuliwa.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Waziri wa Mambo ya nje wa Ghana, Samuel Okudzeto Ablakwa kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X, amesema rais John Dramani Mahama,  ameidhinisha hatua hiyo.

Hatua hii inakuja, baada ya raia wa Ghana wanaoshi nchini Afrika Kusini, kuomba kurejea nyumbani baada ya kuripoti matukio ya kushambuliwa na biashara zao kuvamiwa na kuharibiwa kwa madai kuwa, wageni wamekuja kuchukua ajira wenyeji.

Mwezi uliopita, serikali ya Ghana ilimwita Balozi wa Afrika Kusini jijini Accra, kumhoji kuhusu  matukio hayo ya mashambulizi, yanayoendelea kuchafua jina la taifa hilo lenye wageni zaidi ya Milioni tatu.

Mbali na Ghana, Nigeria pia imechukua hatua hii huku Afrika Kusini, ikikanusha madai ya kuwalinda raia wake wanaowashambulia raia wa kigeni kutoka mataifa ya Afrika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *