Nchini Uganda, rais Yoweri Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 40, ameapishwa tena kuongoza nchi hiyo kwa muhula mwingine wa miaka mitano baada ya kutangazwa mshindi wakati wa uchaguzi mkuu mwezi Januari.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuapishwa, rais Yoweri Museveni alizungumza kuhusu haja ya kuwa na miongozo mipya kupambana na umaskini na ufisadi ambao umekuwa changamoto wakati wa utawala wake.

 “Sasa tunaingia katika muhula mpya. Hakuna tena usingizi na wala rushwa. Familia ambazo zitasikiliza ushauri wetu zitaondoka kwenye umaskini. ” alisema Rais Museveni.

Rais Yoweri Museveni pia alisisitiza haja ya ushirikiano wa kikanda na bara hasa katika biashara ili kujenga utajiri.

Wafuasi wa Rais Museveni wakati wa uapisho wake.
Wafuasi wa Rais Museveni wakati wa uapisho wake. REUTERS – Abubaker Lubowa

Haya hapa ni maoni ya baadhi ya wanainchi kuhusu muhula mpya wa rais Museveni

“Sidhani kama tutakuwana maendeleo kwa sababu ufisadi unaendelea na anatumia pesa nyingi na hatuoni maendeleo yoyote. ” Alieleza mmoja wa raia wa Uganda.

Huku rais Yoweri Museveni akianza muhula mpya madarakani, mpinzani wake mkuu Robert Kyagulanyi Sentamu maarufu kama Bobi Wine bado yuko nje ya nchi akidai aliibiwa.

Kenneth Lukwago Kampala RFI Kiswahili

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *