Ruangwa. Viongozi na wanachama wa vyama vikuu Mkoa wa Lindi   wameendelea kutoa misaada katika hospitali, magereza na wanafunzi wenye mahitaji maalum ikiwa ni kuendeleza ushirika huo katika kurudisha kwa jamii.

Akizungumza mara baada ya kutoa misaada hiyo jana Jumatano Mei 13, 2026 Mwenyekiti wa Jukwaa la Ushirika Mkoa wa Lindi, Odas Mpunga amesema kuwa kutoa misaada hiyo ni kuendeleza kwa sheria ya ushirika namba saba kwa kurudisha kwa jamii kwa kile ambacho wanakipata kwa mwaka mzima.

“Hiki tunachokifanya leo ni sehemu ya kurudisha kwa jamii(Csr)ambapo ushirika namba saba nilazima turudishe kwa jamii nandiyo maana leo tumepeleka vitu mbalimbali katika maeneo yenye uhitaji ikiwemo,hospitali, magereza pamoja na Shule yenye mahitaji maalumu.”amesema Mpunga.

Mmoja wa wagonjwa kutoka hospitali ya Wilaya ya Ruangwa, Salma Bakari amewashukuru vyama vikuu kwa kuwapelekea mahitaji kwani yatawasaidia pindi wanapokuwa hospitalini hapo.

“Tunaushukuru ushirika kwa kuona tunauhitaji wa vitu hapa hospitalini tunawaonba wanaushirika muendelee kutoa misaada hii kila wakati.”amesema Bakari.

Kwa upande wake Mrakibu wa Magereza Wilaya ya Ruangwa, Simion Kanyeshamba amewaomba wadau wengine kujitokeza kutoa misaada kwa watu wenye uhitaji kama walivyofanya wanachama na viongpzi wa ushirika.

“Tunashukuru kwa kupata misaada hii na kuwaomba wadau wengine kujitokeza kusaidia watu wenye uhitaji ili kujenga umoja na mshikamano.”amesema

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *