Msumbiji: Vita vilivyosahaulika vinaendelea kuwatia wasiwasi wakazi wa Cabo DelgadoMsumbiji: Vita vilivyosahaulika vinaendelea kuwatia wasiwasi wakazi wa Cabo Delgado

Kama sehemu ya mfululizo wa ripoti adimu, RFI iliweza kusafiri hadi Cabo Delgado, kaskazini mwa Msumbiji, kwenye mpaka na Tanzania. Kwa karibu miaka kumi, eneo hili limkumbwa na mzozo wa umwagaji damu kati ya kundi lenye silaha la Ahlu Sunnah Wa-Jamma – linalojulikana kama “Al Shabab” – na vikosi vya jeshi la Msumbiji (FADM). Mzozo huu ambao hauzungumziwi sana kwenye vyombo vya habari kutokana na maeneo ambayo hayafikiki, lakini wakazi wanaendelea kulipa gharama kubwa.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu maalum kutoka Mocimboa da Praia:

“Al-Shabaab tayari wanajua mko hapa…” ananong’ona mkuu wa usalama wa shirika lisilo la kiserikali huko Mocimboa da Praia, jiji lililoko kaskazini mashariki mwa Msumbiji. NI hapa ambapo, mnamo mwaka 2017, watu wenye silaha walianzisha mashambulizi dhidi ya vituo kadhaa vya polisi kwa mara ya kwanza. Miaka miwili baadaye, wale wanaojiita Al Shabab waliahidi utii kwa kundi la Islamic State.

“Al Shabab wanataka kulazimisha mfumo wa sheria na mwongozo wa kimaadili wa dini ya Kiislamu (Sharia), lakini pia wanataka mgawanyo bora wa utajiri,” anaelezea João Feijó, mtafiti katika Kituo cha Kuchunguza Mazingira Vijijini. Kundi hili, ambalo linatetea matumizi madhubuti ya Quran, linakadiriwa kuwa na wafuasi mia kadhaa.

Watu kukatwa vichwa, visa vya uporaji na utekaji nyara

Omar Sufo anakumbuka shambulio la mwaka 2017: “Kundi hili la watu wnye silaha liliingia kupitia kitongoji cha Felipe Nyusi. Kiliwakata vichwa watu wanne na kuacha vichwa na miili yao katika maeneo tofauti. Waliporudi, walifanya vivyo hivyo, nyumba kwa nyumba. Waliwaua wanaume na kuwaacha wanawake na watoto.” Kwa wiki kadhaa, Mocimboa da Praia iliendelea kutengwa, huku ikiwa mikononi mwa magaidi.

Fatima Alidi, mjamzito wakati huo, anakumbuka: “Ilikuwa ngumu sana. Nilikuwa na mtoto mwingine wa kiume, mwenye umri wa miaka 10. Sikuweza kukimbia kwa sababu nilikuwa mjamzito. Nilishindwa kufanya majukumu yangu ya kila siku. Nilikuwa nikiteseka sana kiasi kwamba sikujali kama binti yangu alizaliwa akiwa hai au amefariki. Nilitaka tu kuwa huru yaani niweze kutoroka.”

Hali hiyo ya ugaidi inatawala vijijini. Kijiji cha Shute Njojo, mkulima mwenye umri wa miaka 57, kiliharibiwa na Al Shabab: “Watu wenye silaha walinifunga na kuanza kunipiga. Walichukua pesa zangu, mbuzi wangu, na mali zangu zote. Kisha wakachoma nyumba yangu. Nilipofanikiwa kujikomboa, nilikimbilia Palma. Huko, niligundua kuwa magaidi walikuwa wamewateka nyara wajukuu zangu saba.” 

Watu wengine elfu kumi waliokimbia makazi yao

Kwa miaka kadhaa, jiji hili la bandari lenye wakazi 30,000 limekumbwa na uvamizi wa karibu kila wiki: uporaji, mauaji, watukukatwa vichwa, visa vya utekaji nyara, ubakaji… Kiwewe walichokipata wakazi wa Cabo Delgado ni kikubwa.

Mnamo mwezi Septemba 2015, mashambulizi mawili mfululizo yaliikumba Mocímboa da Praia. Simão alikuwa nyumbani kwake wakati watu wenye silaha walipoingia: “Nilijua nia yao ilikuwa kuniua. Kwa hivyo niliamua kukimbia. Nilipendelea kupigwa risasi kuliko kukatwa kichwa. Leo, bado ninaogopa, lakini nafanikiwa kulala.” “Hapo awali, ilikuwa vigumu sana kwangu kulala ndani ya nyumba hapa Mocimboa.”

Pia ikumbukwe kwamba mwanzoni mwa mwezi Mei 2026, watu watano waliuawa katika mashambulizi mawili yaliyofanywa huko Ancuabe na Macomia. Kulingana na shirika lisilo la kiserikali la Acled, angalau watu saba wamepoteza maisha tangu mwisho wa mwezi Aprili, huku Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) likiwa limerekodi zaidi ya watu 12,000 waliokimbia makazi yao tangu mwanzo wa mwezi Mei.

Kutoa msaada wa kisaikolojia kwa waathiriwa

Kwa upande wake, Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) wametekeleza mpango wa afya ya akili katika hospitali ya Mocimboa da Praia. Hatari ni kubwa kwa sababu ukubwa wa mgogoro umesababisha watu kupatwa na mfadhaiko.

“Ikiwa hatua muhimu za afya ya akili hazitachukuliwa sasa, kuna uwezekano mkubwa kwamba tutaona visa vya kujiua, kisaikolojia, na magonjwa mengine katika siku zijazo, kutokana na hali ambayo ianawakabili raai,” anaonya Dkt. Daniel César, mwanasaikolojia.

Karibu watu 210,000 walishiriki katika shughuli za usaidizi wa kisaikolojia wa MSF.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *