Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA), imeridhishwa na maendeleo ya utekelezaji…Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA), imeridhishwa na maendeleo ya utekelezaji…

Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA), imeridhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa Bomba la Kusafirisha Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (EACOP), ikieleza kuwa kasi ya ujenzi ni dalili njema ya kuanza kwa usafirishaji wa mafuta ndani ya muda uliopangwa.

Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya EWURA, Ngosi Mwihava kwa niaba ya wajumbe waliotembelea sehemu ya mradi katika Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera kujionea maendeleo na utekelezaji wa mradi huo wa kimkakati unaounganisha Uganda na Tanzania.

“Ewura ndiyo imetoa kibali cha ujenzi wa bomba hili kwa upande wa Tanzania na ziara hii ilianzia Dodoma ina lengo la kuhakikisha yale yote tuliyokubaliana ikiwamo utunzaji wa mazingira, kutoa kipaumbele cha ajira kwa Watanzania na maeneo mengine yatatekelezwa.”

“Ewura itahusika kutoa vibali pia vya kuanza kazi ya usafirishaji mafuta ghafi kupitia Tanzania, pindi ujenzi wa miundombinu utakapojamilika, hivyo tumeona ni vema kufanya kazi hiyo wakati mradi huu ukiendelea ukingoni,” amesema.

Mradii huo kwa sasa umefikia zaidi ya asilimia 70 huku utekelezaji ikiendelea kwa kasi katika maeneo ya Chongoleani, Tanga ambapo ujenzi wa matenki ya kuhifadhia mafuta ukiwa umekamilika na majaribio yakifanyika.

Mradi wa EACOP unahusisha ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta ghafi lenye urefu wa kilomita 1,443 kutoka Hoima, Uganda hadi Chongoleani, Tanga na sehemu kubwa inapita Tanzania. Unamilikiwa na kampuni ya TotalEnergies kwa asilimia 62, huku Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na Shirika la Mafuta la Uganda (UNOC) kila moja likimiliki asilimia 15 huku kampuni ya CNOOC ya China ikimiliki asilimia nane.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *