Kenya: Serikali na wamiliki wa magari ya usafiri wa umma washindwa kuafikianaKenya: Serikali na wamiliki wa magari ya usafiri wa umma washindwa kuafikiana

Serikali na wamiliki wa magari ya abiria nchini Kenya, wameshindwa kufikia makubaliano kuhusu kusitisha mgomo wa usafiri wa uma, wakati huu watu wanne wakiripotiwa kupoteza maisha hapo jana wakati wa mgomo ulioambatana na maandamano kwenye baadhi ya miji.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika kikao ambacho kilifanyika usiku wa jana, kilitarajiwa kutoka na maazimio ambayo pengine yangeshuhudia mgomo unasitishwa kwa muda au una malizika kabisa kwa serikali kushusha bei ya mafuta kama matakwa ya wadau wa sekta ya Usafiri.

Hata hivyo, majadiliano haya hakuzaa matunda licha ya waziri wa nishati Opiyo Wandayi, kudai kuwa kuna masuala kadhaa walikuwa wameafikiana na wamiliki wa magari ya abiria.

“Tumeelewana kwamba kwa madhumuni ya busara na kuondoa hatari ya uchakachuaji wa mafuta kutokana na tofauti hii kubwa, tutaziba pengo kati ya bei ya dizeli na petroli na hiyo itamaanisha kwamba bei ya mafuta ya taa italazimika kupanda na ile ya dizeli itapungua.” Alisema Waziri Wandayi.

Wamiliki wa magari ya usafiri wa umma wanataka serikali kupunguza bei ya mafuta.
Wamiliki wa magari ya usafiri wa umma wanataka serikali kupunguza bei ya mafuta. REUTERS – Thomas Mukoya

Punde baada ya taarifa yake katika kikao cha pamoja na wanahabari, viongozi wa wamili wa vyombo vya usafiri wa umma, walikana mbele yake kufikia makubaliano yoyote na kusisitiza kuwa mgomo unaendelea.

Albert Karakacha ni mwenyekiti wa muungano huo.

“Kwa hivyo kwa wakati huu  ni ombi letu kwamba madereva na wamiliki wote wa magari waendelea kuweka magari yao nyumbani.” Alisema Albert Karakacha.

Aidha  wadau hao wametoa wito wa mgomo kufanyika kwa njia ya amani, wakisisitiza kuwa watasitisha mgomo huo pale serikali itakaposhusha bei ya mafuta, matakwa ambayo kwa sasa yanaonekana kuwa magumu kutekelezwa na Serikali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *