
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio anaikosoa shirika la Afya Duniani, WHO, kwa “kuchelewa” kutambua mlipuko wa virusi vya Ebola unaoikumba Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hii ni hali nyingine inayozidi kuimarisha mvutano kati ya Marekani na shirika la Afya Duniani (WHO). Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alidai siku ya Jumanne kwamba Shirika la Afya Duniani, ambapo Donald Trump aliiondoa nchi yake kuwa mfadhili wa shirika hilo, lilikuwa “limechelewa kidogo” katika kutambua mlipuko wa virusi vy Ebola unaloathiri Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa sasa.
Alipoulizwa na waandishi wa habari jinsi Marekani ilivyopanga kujibu, mwanadiplomasia huyo mkuu wa Marekani alitangaza: “Wadau wakuu ni wazi watakuwa CDC (Vituo vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa, shirika kuu la afya nchini Marekani), pamoja na Shirika la Afya Duniani, ambalo kwa bahati mbaya lilichelewa kidogo kutambua” mlipuko huu.
Marekani inapanga kufungua kliniki 50 nchini DRC
Marco Rubio pia amebainisha kwamba Marekani, ambayo imetoa dola milioni 13 kama msaada kwa ajili ya shughuli za “mwitikio wa haraka”, inatarajia kufungua kliniki takriban 50 kutibu Ebola nchini DRC, nchi ambayo raia wa Marekani amepimwa na kupatikana na virusi hivyo. “Ni vigumu kidogo kufikia eneo kunakoripotiwa ugonjwa huo kwa sababu ni eneo la vijijini […] na ni mahali pagumu kufikiwa katika nchi iliyoharibiwa na vita, kwa bahati mbaya.” “Tutawekeza sana huko,” Waziri wa Mambo ya Nje ameahidi.
Marekani, chini ya utawala wa Donald Trump, ilijiondoa rasmi kutoka kwa shirika la Afya Duiani, WHO, na kupunguza ufadhili wake kwa Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), ambalo lilihusika pakubwa katika kukabiliana na milipuko ya awali ya Ebola.
Siku ya Jumanne, WHO ilionya kuhusu “kiwango na kasi” ya ugonjwa huu wa Ebola, ambao unashukiwa kusababisha vifo zaidi ya 130, ambao unaenea mashariki mwa DRC.
