Hatima ya afisa wa zamani wa ujasusi wa Austria anayeshtakiwa kwa kuipa taarifa Urusi kujulikanaHatima ya afisa wa zamani wa ujasusi wa Austria anayeshtakiwa kwa kuipa taarifa Urusi kujulikana

Hukumu dhidi ya afisa wa zamani wa idara ya ujasusi anayeshtakiwa kwa kuuza taarifa kwa Urusi inatarajiwa leo Jumatano katika kesi ambayo imechafua sifa ya Austria.

Imechapishwa:

Dakika 3 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Egisto Ott, 63, amekuwa akishtakiwa katika mji mkuu wa Austria tangu Januari 22 kwa shughuli zilizofanywa bila kibali kati ya mwaka 2015 na 2022, kulingana na upande wa mashtaka, ambao ulifanya uchunguzi kwa zaidi ya miaka minane na kukawasilisha mashtaka zaidi ya kumi na mawili, ikiwa ni pamoja na ujasusi dhidi ya Austria.

Anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka mitano jela.

Kesi ya upande wa mashtaka inategemea sehemu ya ushahidi uliotolewa kwa Austria na nchi ya Magharibi, ambayo ilimgundua Ott wakati wa uchunguzi. Shahidi kutoka Uingereza alitoa ushahidi katika kesi hiyo.

Kulingana na mahakama, jopo la majaji litajadili kwa saa kadhaa, na uamuzi huo unatarajiwi kabla ya saa sita mchana.

Egisto Ott, aliyehojiwa na shirika la habari la AFP siku ya  Jumanne, alikataa mashtaka yote, akisema “hana hatia.” “Hakuna wakati wowote nilipouza au kusambaza taarifa yoyote kwa idara za ujasusi za Urusi,” alisema, akibainisha kwamba alikuwa akifanya kaei yake kila mara kwa amri kutoka kwa wakubwa wake au kwa mamlaka ya kisheria.

Kulingana na mashtaka yaliyopitiwa na AFP, inadaiwa “alituma maombi ya usaidizi wa kisheria wa pande zote” kwa Italia na Uingereza, jambo lililosababisha zitende “bila ridhaa yao kwa maslahi” ya Moscow. Inasemekana alifanya hivyo kwa amri ya Jan Marsalek, kiongozi wa zamani wa Austria wa shirika la Wirecard la Ujerumani, anayetafutwa kwa ulaghai, anayedhaniwa kuwa mkimbizi nchini Urusi, na anayeshukiwa kufanya kazi kwa idara ya Usalama ya Shirikisho la Urusi (FSB).

Inadaiwa alikabidhi simu za mkononi za maafisa watatu wa ngazi za juu katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Austria, ambazo, miongoni mwa mambo mengine, zilihatarisha usalama wa wakimbizi wa Ukraine na Chechnya nchini Austria, huku pia zikifichua maelfu ya mawasiliano yaliyohifadhiwa kwenye vifaa hivyo.

– Kiota cha wapelelezi –

Kipakatalishi “ambacho kumehifadhiliwa vifaa vya usalama vya kielektroniki visivyojulikana hadharani vinavyotumiwa na mataifa ya EU kwa mawasiliano salama ya kielektroniki” pia inadaiwa kilipewa FSB. Kisha kiliripotiwa kuuzwa kwa Iran.

Egisto Ott pia inadaiwa alisambaza taarifa kuhusu watu “waliotishiwa kulipiza kisasi” nchini Urusi, kama vile jasusi wa zamani wa Urusi ambaye alikuwa amekimbilia Montenegro. Pia alitoa msaada kwa njia isiyo ya moja kwa moja kwa Arkady Rotenberg, mshirika wa karibu wa Rais wa Urusi Vladimir Putin, ambaye alikuwa chini ya vikwazo vya Ulaya.

Hakika, Moscow ilikuwa ikijaribu kujua ni kwa nini mpenzi wa mfanyabiashara huyo Mlatvia alikuwa akipitia matatizo kuvuka mipaka ya Ulaya.

Wachunguzi pia walipata uchambuzi muhimu ambao Bw. Ott aliandika kuhusu utaratibu wa mauaji ya mwaka 2019 ya mwanamume Mgeorgia mwenye asili ya Chechen huko Berlin na wakala aliyetumwa na Moscow.

Afisa mwingine wa Austria anashtakiwa pamoja naye, ambaye anadai hakujua kamwe kwamba taarifa ambayo Egisto Ott aliomba ilikusudiwa Urusi.

Zaidi ya miaka minne baada ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Vienna bado inaelezewa mara kwa mara kama kitovu cha wapelelezi wa Urusi, na wafanyakazi wapatao 220 bado wana vibali vya ubalozi wa Urusi, ​​moja ya misheni kubwa zaidi za kidiplomasia za Urusi barani Ulaya.

Nchini Austria, ujasusi unabaki kuwa halali mradi tu hautatekelezwa kwa madhara ya maslahi ya nchi mwenyeji, jambo ambalo limeathiri uhusiano kati ya taifa hili lenye wakazi milioni 9.2 na idara zake za ujasusi katika miaka ya hivi karibuni.

Ili kuwanyamazisha wakosoaji, serikali ya muungano kati ya wahafidhina, sicial Democratic na waliberali inafikiria kupanua msako huo hadi ujasusi dhidi ya EU au mashirika ya kimataifa yaliyoko Vienna na kuadhibu zoezi la kuajiri maafisa wa idara za ujasusi za kigeni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *