Trump: Mazungumzo na Iran yako katika hatua za mwisho, tutawashambulia iwapo hawataafikia makubalianoTrump: Mazungumzo na Iran yako katika hatua za mwisho, tutawashambulia iwapo hawataafikia makubaliano

Picha ya Donald Trump

Chanzo cha picha, Getty Images

Rais wa Marekani Donald Trump amesema
atazungumza na kiongozi wa Taiwan, Lai Ching-te, kuhusu uwezekano wa kuiuzia Taiwan silaha, hatua ambayo ni mabadiliko makubwa kutoka utamaduni wa
kidiplomasia uliodumu kwa miaka mingi katika kisiwa hicho na
Marekani.

Viongozi wa Marekani na Taiwan hawajawahi
kuzungumza moja kwa moja tangu mwaka wa 1979, wakati Washington ilipositisha rasmi uhusiano wake na Taiwan ili kuitambua
serikali ya Beijing kama serikali halali ya China.

Beijing inaichukulia Taiwan kama sehemu ya
himaya yake na haijaondoa uwezekano wa kuitwaa kwa nguvu za kijeshi.

Lai, aliingia madarakani mwaka wa 2024, na ameongoza moja ya juhudi kubwa zaidi katika
miaka ya hivi karibuni za kuimarisha ulinzi wa kisiwa hicho.

Marekani kwa muda mrefu imekuwa ikiunga mkono
Taiwan na kuipatia silaha za kujilinda, lakini imekuwa ikijaribu kudumisha
uhusiano wa kidiplomasia na China.

Alipoulizwa na wanahabari iwapo anapanga kuzungumza na Lai,
kuhusu kuiuzia Taiwan silaha, Trump alisema, “nitazungumza naye. Nazungumza na kila mtu tutalifanyia kazi hilo, tatizo la Taiwan.”

Katika
ziara yake ya hivi karibuni nchini Taiwan, Rais Xi Jinping wa China alitaka Marekani kusitisha uuzaji wa silaha kwa Taiwan.

Mwaka wa 1979, Marekani ilipitisha Sheria ya Mahusiano
na Taiwan inayoruhusu Marekani kuipatia Taiwan silaha za kujilinda, sheria ambayo inatumika kuiuzia
Taiwan silaha hadi leo.

Pia unaweza kusoma:

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *