
Mkutano mkuu wa All Progressives (APC), chama cha rais wa Nigeria anayemaliza muda wake, umemteua rasmi kupeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi wa urais utakaofanyika Januari 16 nchini Nigeria. Bola Ahmed Tinubu, ambaye hajaficha nia yake ya kugombea muhula wa pili, kwa sasa anapewa nafasi kubwa ya kushinda katika uchaguzi huo.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Lagos, Harmony Pondy Nyaga
Kufuatia kura za mchujo zilizopigwa ndani ya chama chake, rais wa Nigeria anayemaliza muda wake, Bola Ahmed Tinubu, aliteuliwa rasmi siku ya Jumapili, Mei 24, kama mgombea wa All Progressives Congress (APC) katika uchaguzi wa urais wa mwezi Januari 2027. Anachukuliwa kuwa mgombea anayepewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo kutokana na usaidizi aliopokea kutoka kwa magavana 31 kati ya 36 wa nchi hiyo, pamoja na kuwa kwa sasa anakabiliwa na upinzani uliogawanyika.
Katika sherehe iliyofanyika katika mji wa Abuja, akiwa amevaa kofia yake ya kitamaduni ya Kiyoruba—alipokea bendera ya chama chake na cheti chake cha kuteuliwa tena kwa muhula mpya wa miaka minne. “Ninarudi leo kama rais anayemaliza muda wake, nikiguswa na uungwaji wengu mkono usiyotetereka, nikitiwa moyo na imani yenu thabiti, na nimejaa shauku mpya kwa changamoto zilizo mbele,” alitangaza katika hafla hiyo.
Zaidi ya kura milioni 10
Kati ya wapiga kura takriban milioni 11, Bola Ahmed Tinubu alipata zaidi ya kura milioni 10, ikilinganishwa na zaidi ya kura 16,000 kwa mpinzani wake pekee, mfanyabiashara asiyejulikana sana, Stanley Osifo. Mbali na wanaharakati wa APC, mageuzi ya kiuchumi aliyotekeleza na ukuaji uliotangazwa wa zaidi ya 4% mnamo mwaka 2026 yamewashawishi baadhi ya Wanigeria, kama Furo Heart, mbunifu wa mambo ya ndani. “Ninahisi kwamba pamoja naye, kwa njia moja au nyingine, tutafanikiwa. Kwa sasa, nitafuata tu ‘baba’: tayari amekuwa madarakani, anajua jinsi ya kufanya mambo. Kwa hivyo hatuhitaji mtu ambaye hajakuwa na uzoefu,” anasema.
Hata hivyo, mnamo mwezi Januari, rais aliye madarakani pia atalazimika kujibu kwa rekodi isiyo ya ajabu katika sanduku la kura, kuanzia na mfumuko wa bei unaozidi 15% tangu mwanzo wa mwaka 2026, ambao unaathiri vibaya ubora wa maisha kwa Wanigeria, pamoja na hali ya usalama inayoendelea kuwa mbaya. Hii inatokana hasa na kuibuka tena kwa mashambulizi kutoka kwa magenge ya wahalifu na makundi ya wanajihadi kaskazini mwa nchi.
Orodha kamili ya wagombea wa uchaguzi wa urais wa Januari 16, 2027 inatarajiwa Mei 31 nchini Nigeria.
