Papa Leo aomba radhi kutokana na nafasi ya Kanisa Katoliki katika biashara ya utumwa ya kuvuka Bahari ya AtlantikiPapa Leo aomba radhi kutokana na nafasi ya Kanisa Katoliki katika biashara ya utumwa ya kuvuka Bahari ya Atlantiki

Katika hatua ya kihistoria, Papa Leo wa XIV Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani ameomba radhi kutokana nafasi ya Baraza Kuu la Uongozi wa Kanisa Katoliki na Jiji la Vatican la kuhalalisha utumwa na kushindwa kulaani suala hilo kwa karne kadhaa.

Kiongozi huyo wa Kanisa Katoli Duniani ameitaja rekodi hiyo ya Vatican kuwa “jeraha katika kumbukumbu ya Kikristo.”

Mapapa wa Kanisa Katoliki waliotangulia waliomba radhi kufuatia kuhusika Wakristo katika biashara ya utumwa ya kuvuka Bahari ya Atlantiki, lakini hakuna Papa yoyote aliyewahi kujitokeza hadharani na kukiri kuhusu suala hilo hadi kiasi cha kuomba radhi; dhima ambayo ilibebewa na mapapa wa zamani ambao waliwapa watawala wa Ulaya mamlaka ya wazi ya kuwafanya mamilioni ya watu kuwa watumwa, hasa Waafrika.

Leo wa XIV ni Papa wa kwanza mzaliwa wa Marekani katika historia, ambaye historia ya familia yake inajumuisha watu waliokuwa watumwa na wamiliki wa watumwa, jana Jumatatu aliomba radhi kupitia waraka wake wa kwanza, (Magnificent Humanity), uliotolewa siku hiyo.

Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani amesema: Kwa kufanya hiyo nimeitikia wito wa miongo kadhaa wa Wakatoliki weusi wa Marekani, wanaharakati na wasomi waliotaka Baraza Kuu la Uongozi wa Kanisa Katoliki na Jiji la Vatican kubeba dhima ya biashara ya utumwa, enzi za ukoloni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *