Maonesho ya kuenzi maisha na urithi wa mwanadiplomasia mashuhuri wa Tanzania, Dkt. Salim Ahmed Salim, yamefungua mjadala mpana kuhusu mwelekeo wa maendeleo ya bara la Afrika.
Maonesho hayo yaliyofunguliwa Mei 25, 2026 jijini Dar es Salaam, yanaangazia mabadiliko ya fikra kutoka harakati za kisiasa kuelekea diplomasia ya maendeleo na ukuaji wa uchumi.
Akizungumza katika mjadala wa ufunguzi, Balozi John Ulanga amesema kizazi cha viongozi wa awali kilijikita katika kujenga umoja na misingi ya kisiasa, huku sasa mkazo ukiwa katika kukuza uchumi wa mataifa ya Afrika.
Kwa upande wake, Ahmed Salim ambaye ni mtoto wa Dkt. Salim amesema maonesho hayo yanaonesha mchango wa Tanzania katika mijadala ya kimataifa na kuimarisha uelewa wa diplomasia ya Afrika.
Maonesho hayo ya mwezi mmoja yanajumuisha nyaraka, hotuba na kumbukumbu muhimu za kidiplomasia zinazoakisi mchango wa Dkt Salim Ahmed Salim katika jukwaa la kimataifa.
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates
(Feed generated with FetchRSS)
