Saturn Corporation yazindua uunganishwaji wa magari ya pick up nchiniSaturn Corporation yazindua uunganishwaji wa magari ya pick up nchini

Dar es Salaam. Kampuni ya Saturn Cooperation imezindua upanuzi wa kiwanda chao  cha uunganishaji magari kilichopo  Kigamboni  Wilaya ya Kigamboni ili kuwezesha kuanza rasmi kwa shughuli za kuunganisha magari ya pick-up na magari mengine madogo ya kubeba mizigo hapa Tanzania.

Uzinduzi huo ulifanyika jana Jumapili Mei 24,2026 kiwandani hapo na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara wa magari na wale waliopo katika  sekta ya usafirishaji.

Katika ufanyaji wa shughuli hiyo, Saturn Cooperation imeingia makubaliano ya ushirikiano na kampuni ya Sinotruk.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Rehmatullah Habib, amesema moja ya magari yatakyounganisha ni aina ya Sinotruk Bolden ambayo, hatua inayochochea ukuaji wa viwanda, uhamishaji wa teknolojia na uundaji wa ajira kwa Watanzania.

Habib amesema kupitia ushirikiano huo na Sinotruck, kampuni yao itananua shughuli zake katika makundi mengine ya magari ikiwemo pick-up,na magari yenye uzito mwepesi pamoja na magari maalum ya kibiashara,.

“Hatua hii itaongeza zaidi ajira, kuimarisha utaalamu wa kiufundi na kuchangia kwa kiwango kikubwa katika uchumi wa viwanda wa nchi yetu,”amesema.

“Hivyo tunapotia saini ushirikiano huu leo, tunathibitisha tena dhamira yetu ya kuendelea kuunga mkono ajenda ya Tanzania ya viwanda na kuchangia kwa maana katika ukuaji wa uchumi, uundaji wa ajira, uhamishaji wa teknolojia pamoja na maendeleo endelevu.

Hata hivyo amesema tangu kuzinduliwa kwa kiwanda hicho nchini, mafanikio yamekuwa makubwa zaidi ya shughuli za kuunganisha malori pekee, mafanikio ambayo ni wazi  yanaakisi ukuaji wa utaalamu wa ndani, kuongezeka kwa imani katika uwezo wa viwanda vya Tanzania.

“Katika kipindi cha miaka miwili pekee, Saturn Corporation imefanikiwa kutoa ajira moja kwa moja kwa zaidi ya Watanzania 360 kutoka 155 na wasio rasmi 2500, wengi wao wakiwa vijana waliopatiwa mafunzo katika uunganishaji wa magari, uhandisi na shughuli za uzalishaji viwandani.

“Leo hii, vijana hawa wanaendesha kwa ufanisi mkubwa mifumo ya kisasa ya uunganishaji ambapo hapo awali ilitegemea kwa kiasi kikubwa wataalamu wa kigeni.

Kwa upande wa uwekezaji amesema kupitia teknolojia umeleta ukuaji mkubwa wa kiutendaji ambapo hicho kina uwezo kuunganisha hadi malori makubwa 30 kwa sikubkutoka kumi, sawa na zaidi ya malori 650 kwa  mwezi.

Katika hatua nyingine, ameipongeza Serikali kwa kuendelea kuwekeza katika miundombinu wezeshi ikiwemo upanuzi wa vituo vya kujazia gesi ya CNG ambavyo vitakuwa muhimu katika kusaidia mabadiliko haya kuelekea usafiri safi na wenye gharama nafuu zaidi.

“Mpango huu hauendani tu na vipaumbele vya kimataifa vya mazingira, bali pia unalenga kupunguza gharama za uendeshaji kwa wasafirishaji na viwanda huku ukiunga mkono azma ya Tanzania katika matumizi ya nishati safi,”amesema Habib.

Akielezea kuhusu changamoto, Mkurugenzi hiyo amesema ili kuweza kufikia lengo la kupanua uzalishaji wa malori, bado kunahitajika mazingira wezeshi ya kikodi yatakayofanya magari yanayounganishwa nchini kuwa na bei rafiki zaidi ikilinganishwa na magari chakavu yanayoingizwa kutoka nje.

Ili kulitekeleza hili amesema kuna haja ya serikali kuweka sera zitakazopunguza ushindani kwa magari ya mitumba ili kukuza bidhaa ya “Made in Tanzania”.

Jingine ametaka kuendelea kurahisisha taratibu za bandarini ili malighafi zifike kiwandani kwa wakati.

Kwa upande wake

Meneja Mkuu wa Kitengo cha Afrika Mashariki wa Sinotruk,Tony Jia amesema hapo nyuma katika miaka ya 1970, malori 731 ya Sinotruk Huanghe yalitumika katika ujenzi wa reli ya  Tazara, yakibaki kuwa ushahidi wa kudumu wa urafiki kati ya China na Tanzania.

Jia amesema katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, Sinotruk imesambaza zaidi ya malori 30,000 nchini Tanzania, yakiambatana na kushuhudia ukuaji mkubwa wa taifa hili.

“Kwa kujikita katika kukuza viwanda vya ndani, Sinotruk ilianzisha ushirikiano wa kimkakati na Saturn nchini Tanzania mwaka 20…

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *