Ujumbe wa Hija: Kiongozi Muadhamu ayatolea wito mataifa ya Kiislamu kuunda utaratibu mpya wa kikanda; asema enzi ya US imefikia tamatiUjumbe wa Hija: Kiongozi Muadhamu ayatolea wito mataifa ya Kiislamu kuunda utaratibu mpya wa kikanda; asema enzi ya US imefikia tamati

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Sayyid Mojtaba Khamenei amezitolea wito nchi za Kiislamu kuzidisha ushirikiano na kuanzisha utaratibu mpya wa kieneo na kimataifa mbali na utawala wa Marekani.

“Umma [ulimwengu] wa Kiislamu na mataifa ya eneo hili yana uwezo mkubwa na maslahi ya pamoja ambayo yatapelekea kuasisiwa utaratibu mpya na usanifu wa siku zijazo wa eneo la Asia Magharibi na ulimwengu mzima kwa ujumla,” ameeleza Ayatollah Mojtaba Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi katika ujumbe wake alioutoa leo kwa Mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu.

Ujumbe huu ambao umetolewa kwa mnasaba wa Siku ya Arafa, siku ya pili ya ibada ya Hija, umeeleza kuwa mataifa ya Kiislamu yanaingia katika awamu ya kihistoria huku hali halisi ya ukweli wa mambo katika eneo ikibadilika kikamilifu, na ushawishi wa kijeshi wa Marekani ukizidi kupungua.

Ayatullah Mojtaba Khamenei amesema kuwa ushawishi uliokuwepo huko nyuma hautakaririwa tena; na nchi za kanda hii hazitatumika tena kama ngao za kambi za kijeshi za Marekani.

“Marekani “haitakuwa tena na mahali salama pa kufanyia uovu wake na kuanzisha vituo vya kijeshi katika kanda hii’ amesema Kiongozi Muadhamu katika ujumbe wake kwa Mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu.

Ujumbe huu wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu umeangazia mchango wa kambi ya muqawama katika eneo, ambapo ameitaja kambi hiyo kama harakati ya umoja na mshikamano iliyopanuka kuanzia Iran hadi Lebanon na Palestina, Iraq na Syria, kuanzia Afrika na Yemen hadi Afghanistan na Pakistan.”

Ujumbe kamili wa Ayatullah Mojtaba Khameneoi utawajia baada ya taarifa ya habari za dunia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *