Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Abdulaziz (KAIA) uliopo Jeddah nchini Saudi Arabia umeendelea kuwa mhimili muhimu katika ku…Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Abdulaziz (KAIA) uliopo Jeddah nchini Saudi Arabia umeendelea kuwa mhimili muhimu katika ku…

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa King Abdulaziz (KAIA) uliopo Jeddah nchini Saudi Arabia umeendelea kuwa mhimili muhimu katika kurahisisha ibada ya Hijja, ukihudumia mamilioni ya mahujaji kutoka mataifa mbalimbali duniani wanaoelekea mji mtakatifu wa Makka kila mwaka.

Katika miaka ya hivi karibuni, uwanja huo umefanyiwa maboresho makubwa ya miundombinu na huduma kupitia mfumo wa ubia kati ya sekta ya umma na binafsi, hatua iliyoongeza kwa kiasi kikubwa ufanisi wa huduma kwa mahujaji.

Maboresho hayo yamewezesha kupungua kwa muda wa kukamilisha taratibu za uwanjani kutoka kati ya saa sita hadi kumi hapo awali, hadi wastani wa dakika 45 hadi saa moja kwa sasa.

Aidha, uwezo wa uwanja huo umeongezeka kutoka kuhudumia takribani mahujaji milioni moja kwa mwaka hadi kati ya abiria milioni nane na tisa kwa mwaka, jambo linalochangia kupunguza msongamano na kurahisisha safari za ibada hiyo muhimu kwa Waislamu.

Akizungumzia mafanikio hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia kati ya Sekta ya Umma na Binafsi (PPP), David Kafulila, amesema mageuzi hayo yanaonesha namna uwekezaji wa ubia unavyoweza kuboresha kwa haraka huduma za miundombinu mikubwa.

Kafulila amesema mradi huo wenye thamani ya dola milioni 249 ulitekelezwa kupitia ushirikiano kati ya Mamlaka ya Anga ya Saudi Arabia na sekta binafsi, ukihusisha wadau mbalimbali wa kimataifa, hatua iliyowezesha kuleta mabadiliko makubwa katika usimamizi na utoaji wa huduma za uwanja huo.

Kwa mujibu wa takwimu za kimataifa za mwaka 2023, viwanja vya ndege vinavyoendeshwa kwa mfumo wa PPP vinachangia takribani asilimia 14 pekee duniani, lakini vinahudumia karibu asilimia 40 ya abiria wote, hali inayoonesha mchango mkubwa wa mfumo huo katika kuboresha huduma za usafiri wa anga duniani.

Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *