Wanafunzi 16 wafariki dunia Kenya baada ya moto kuteketeza bweni Utumishi Girls AcademyWanafunzi 16 wafariki dunia Kenya baada ya moto kuteketeza bweni Utumishi Girls Academy

Wanafunzi 16 wameuawa baada ya moto kuteketeza bweni lao usiku wa kuamkia leo katika shule ya bweni huko Gilgil, (Utumishi Girls Academy) yapata kilomita 120 (maili 77) magharibi mwa mji mkuu wa Kenya, Nairobi, mamlaka imethibitisha.

Waziri wa Kenya, Elimu Julius Ogamba ambaye ametembelea eneo la moto amesema makumi ya wanafunzi wengine wamejeruhiwa na kupelekwa hospitalini. 71 kati ya majeruhi hao waliruhusiwa baadaye na saba wamelazwa kwa matibabu zaidi.

Moto huo uliotokea katika Chuo cha Wasichana cha Utumishi ulianza mapema leo Alhamisi wakati wanafunzi walipokuwa wamelala.

Waziri wa Elimu wa Kenya amesema moto huo uliibuka kwenye ghorofa ya kwanza ya moja ya mabweni, ambayo “yaliharibiwa kabisa” katika moto huo.

“Timu za kukabiliana na moto zilifanikiwa kuzima moto huo kufikia saa 9 alifajiri, lakini kufikia wakati huo uharibifu ulikuwa tayari umetokea,” amesema Julius Ogamba.

Ameongeza kuwa shule hiyo itaanza kuwakabidhi wanafunzi kwa wazazi na walezi wao huku mamlaka zikiendelea na uchunguzi.

Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Kipchumba Murkomen, ambaye pia alikuwa miongoni mwa maafisa waliokusanyika shuleni hapo, ametuma salamu zake za rambirambi kwa familia za wanafunzi wliofariki dunia.

“Ni wakati wa wasiwasi sana na hata tunapozungumzia watu 16 waliotambuliwa hadi sasa kuwa wamefariki dunia, nataka kuwaomba watu wa Kenya kwamba kwa pamoja tusimame na familia katika maombi, katika usaidizi.”

Matukio ya moto si jambo la kawaida katika shule za bweni za Kenya, na matukio kadhaa ya vifo yameripotiwa katika miaka ya hivi karibuni. Mengi yamekuwa matokeo ya uchomaji moto, huku wanafunzi waliokuwa na hasira kuhusu nidhamu na hali ya maisha – wakituhumiwa kuhusika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *