Kituo cha kuwahifadhi Wamarekani walioambukizwa Ebola kufunguliwa KenyaKituo cha kuwahifadhi Wamarekani walioambukizwa Ebola kufunguliwa Kenya

Kituo cha kuwahifadhi raia wa Marekani walioambukizwa virusi vya ebola, kinatarajiwa kufunguliwa nchini Kenya hivi leo, kwa mujibu wa maafisa wa Marekeni ambao wametetea uamuzi wa Washington uliokashifishwa wa kutowarejesha nyumbani raia wao wlioambukizwa virusi hivyo.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kituo hicho kilichojengwa na Marekani katika kambi ya kijeshi eneo la Laikipia, kinatarajiwa kuwaweka karantini raia wa Marekani ambao huenda wakawa wametangamana na watu waliaombukizwa virusi vya Bundibugyo ambavyo vimesababisha mlipuko mpya wa Ebola.

Afisa mmoja wa Marekani ambaye hakutaka kutambuliwa, amesema kituo hicho kitakuwa na vitanda 50 vya kuwatenga raia hao na kitasimamiwa na wafanyakazi wa afya wa Marekani ambao wanatarajiwa kuwasili nchini Kenya.

Baadaye, maeneo mengine matatu ya watu kutengwa yataongezwa, kila eneo likiwa na uwezo wa kuwahifadhi wagonjwa wanne, lengo likiwa kuwatenga Wamarekani ambao wanaamikia kutangamana na wagonjwa wa ebola katika mataifa ya DRC na Uganda.

Aidha afisa huyo amesema kuwa iwapo wagonjwa hao wataonesha dalili au kupatikana wameambukizwa Ebola, basi watatibiwa kwenye kituo hicho hadi pale watakaposafirishwa katika vituo maalum barani Ulaya.

Kulingana na afisa huyo, Marekani imechukua hatua ya kufungua kituo hicho nchini kenya, ili kupisha safari ya wagonjwa hao, huu akikanusha kuwa ni hatua iliochochewa kisiasa.

Hayo yakijiri, shirika moja la kuteta haki za binadamu nchini Kenya limewasilisha kesi mahakamani kupinga mpango kuwepo kwa kituo hicho cha karantini, kwa msingi kwamba mpango huo umefanyika kwa siri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *