Togo: WFP yaonya kuhusu ukosefu wa usalama wa chakula kaskazini mwa nchiTogo: WFP yaonya kuhusu ukosefu wa usalama wa chakula kaskazini mwa nchi

Nchini Togo, zaidi ya watu 330,000 wanaweza kukabiliwa na ukosefu wa usalama wa chakula katika miezi mitatu ijayo ikiwa hawatapokea msaada, kulingana na makadirio ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) katika hati iliyochapishwa siku chache zilizopita. Maeneo yaliyo kaskazini mwa nchi ndio mahali ambapo mahitaji makubwa zaidi yamejikita, yakizidishwa na hali ya usalama.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Eneo la Savanes ndilo lililo hatarini zaidi, kulingana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani. Eneo hili, linalopakana na Burkina Faso na linalokabiliwa na tishio la kigaidi, bado liko katika hali ya dharura ya usalama. Hali hii wakati mwingine inaweza kuvuruga upatikanaji wa masoko katika maeneo ya mpakani na kusababisha watu kuhama makazi yao.

WFP imerekodi wakimbizi 50,000 na zaidi ya watu 10,000 ambao ni wakimbii wa ndani. Takwimu hizi ni za mwisho wa mwezi uliopita.

Katika kaskazini mwa nchi, msimu wa kiangazi ulianza mwezi uliopita. Akiba ya chakula inapungua kwa kasi, inaelezea WFP, na uwepo wa wakimbizi na watu waliohamishwa ndani ya nchi unazidisha shinikizo la rasilimali. Kwa hivyo, WFP inaelekeza shughuli zake kwa watu hawa walio katika mazingira magumu na jamii zinazowahifadhi.

Hali ya hewa ngumu

Shirika hilo pia linaangazia changamoto za hali ya hewa zinazoikabili nchi: mvua inayonyesha vibaya, wakati mwingine mafuriko, na uharibifu wa ardhi unaofanya uzalishaji wa kilimo kuwa mgumu.

Mambo haya, pamoja na bei ya juu ya chakula, kulingana na WFP, hupunguza upatikanaji wa chakula chenye lishe kwa kaya zilizo katika mazingira magumu zaidi.

Utafiti, uliozinduliwa mwaka jana na serikali ya Togo na kuchapishwa mwezi mmoja uliopita, unahitimisha kuwa 50% ya familia haziwezi kumudu lishe bora.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *