Messi uhakika Kombe la Dunia, Argentina ikianika kikosiMessi uhakika Kombe la Dunia, Argentina ikianika kikosi

Argentina imeanika kikosi chake cha wachezaji 26 watakaoshiriki Fainali za Kombe la Dunia mwaka huu wakiongozwa na mshambuliaji mkongwe na tegemeo, Lionel Messi.

Kulikuwa na wasiwasi juu ya hali ya kiafya ya Messi baada ya kupata maumivu ya misuli katika mechi ya Ligi Kuu Marekani dhidi ya Philadelphia Union, Jumapili iliyopita ambayo hakuweza kumaliza.

Hata hivyo, maumivu yanaonekana hayatokuwa ya muda mrefu kiasi cha kumfanya Messi akose Kombe la Dunia na Argentina kama ilivyotegemewa imemjumuisha kundini nyota huyo wa Inter Miami.

Wachezaji sita walioitwa katika kikosi hicho cha Argentina, wanaitumikia Atletico Madrid inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania ‘La Liga’ jambo linaloifanya iwe klabu iliyotoa idadi kubwa ya wachezaji katika kikosi cha Argentina.

Kocha Lionel Scaloni amewajumuisha makipa, Juan Musso (Atletico Madrid), Geronimo Rulli (Marseille) na Emiliano Martinez (Aston Villa).

Upande wa mabeki kuna Leonardo Balerdi (Marseille), Nicolas Tagliafico (Lyon), Gonzalo Montiel (River Plate), Lisandro Martinez (Manchester United), Cristian Romero (Tottenham), Nicolas Otamendi (Benfica), Facundo Medina (Marseille) na Nahuel Molina (Atletico Madrid).

Kikosi kitakuwa na viungo Leandro Paredes (River Plate), Rodrigo de Paul (Inter Miami), Valentin Barco (Strasbourg), Giovani lo Celso (Real Betis), Ezequiel Palacios (Bayer Leverkusen), Alexis Mac Allister (Liverpool) na Enzo Fernandez (Chelsea).

Washambuliaji walioitwa ni Julian Alvarez (Atletico Madrid), Lionel Messi (Inter Miami), Nicolas Gonzalez (Atletico Madrid), Thiago Almada (Atletico Madrid), Giuliano Simeone (Atletico Madrid), Nico Paz (Como), Jose Manuel Lopez (Palmeiras) pia Lautaro Martinez (Inter Milan).

Katika Kombe la Dunia 2026, Argentina imepangwa kundi J ambalo pia linazijumuisha timu za Algeria, Austria na na Jordan.

Itaanza mashindano hayo kwa kuikabili Algeria, Juni 17, kisha itacheza na Austria, Juni 22 na  itakabiliana na Jordan, Juni 28.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *