Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando imeanza kutoa fursa kwa wauguzi wake kujiendeleza kielimu hadi ngazi za ubingwa, hatua inayolenga kuimarisha utoaji wa huduma kwa wagonjwa.

Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Sister Alicia Masenga, amesema mpango huo ni sehemu ya juhudi za kuongeza ubora wa huduma za afya katika hospitali hiyo.

Akizungumza katika kilele cha maadhimisho ya Siku ya Wauguzi jijini Mwanza, amesema pia hospitali inaendelea kuboresha mazingira ya kazi kwa kuimarisha miundombinu ili kuwawezesha wauguzi na wataalamu wengine kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

Kwa upande wake, Chama cha Wauguzi Tanzania tawi la Bugando kimesema kinaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali, ikiwemo ujenzi wa chuo cha wauguzi wilayani Misungwi.

✍ Innocent Aloyce
Mhariri @claud_jm
#AzamTVUpdates

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *