#HABARI: Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Patrobas Katambi amewasihi askari polisi kulinda viapo hata baada ya kustaafu utumishi katika Jeshi la Polisi huku akiwapongeza wahitimu Mia Saba Kumi na Tisa waliohitimu Kozi Namba Moja ya Mwaka 2025/2026 katika Chuo cha Taaluma ya Polisi, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mbele ya Rais alimuahidi Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan utii usiogawanyika katika utekelezaji wa majukumu yote ambayo Wizara na Vyombo vyake vya Usalama wamepatiwa kuyatekeleza huku akiahidi uwepo wa nidhamu na kuhakikisha wale ambao wanaenda kinyume hatua zinachukuliwa dhidi yao.

Waziri Katambi aliwakumbusha na kuwasihi askari kuishi katika viapo vyao ambapo askari wengi wamekuwa wakiishi katika viapo vyao na kufuata misingi.

Waziri huyo pia aliiasa jamii juu ya wahalifu akiweka wazi wahalifu kutoka katika familia na watu wema pia wakitokea katika familia ambapo aliziomba taasisi za dini na familia kuendelea kumsaidia Mheshimiwa Rais kulinda maadili ya taifa huku mmomonyoko wa maadili ukiwa ndio chanzo cha uhalifu na masuala mengine yanayoweza kulidhuru taifa la Tanzania.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *