Marekani imetangaza vikwazo kwa Makamanda wa makundi yenye silaha inayoyatuhumu kwa kuwa nyuma ya mapigano yanayoendelea mashariki ya Kongo licha ya juhudi za upatanishi wa Washington.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Makabiliano yamekuwa yakiripotiwa mashariki ya Kongo kati ya waasi wa M23 ambao Umoja wa Mataifa unasema wanaungwa mkono na Rwanda na wapiganaji wa FDLR.

Makamanda waliotangaziwa vikwazo ni pamoja na John Imani Nzenze wa kundi la M23 ambaye pia anahudumu kama afisa wa intelejensia wa kundi hilo na Gustave Kubwayo wa kundi la FDLR.

Rwanda na Congo zilitia saini makubaliano ya amani jijini Washington mwezi Disemba mwaka wa 2025 kama sehemu ya juhudi za Rais Trump kujaribu kupata mwafaka kumaliza mzozo wa mashariki ya Kongo.

Licha ya makubaliano hayo, waasi wa M23 waliingia katika Mji wa Uvira Mashariki ya Kongo kwenye mpaka na nchi ya Burundi kabla ya kuondoka kwa shinikizo la Marekani.

Mapigano Mashariki ya DRC yamesababisha mamilioni ya raia kuyahama makazi yao wakati maelfu ya wengine wakiuawa kwenye makabiliano kati ya wanajeshi wa serikali na makundi yenye silaha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *