Baraza la Wawakilishi la Marekani limeidhinisha azimio linalolenga kupunguza mamlaka ya vita ya Rais Donald Trump kuhusiana na Iran, ikiwa ni ishara ya changamoto kubwa kwa jinsi utawala wa Trump unavyoshughulikia uchokozi wake dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu.

Hatua hiyo ilipitishwa jana Jumatano kwa kura ya 215-208, huku Wawakilishi wa Republican Thomas Massie, Brian Fitzpatrick, Tom Barrett, na Warren Davidson wakijiunga na Democrats katika kuunga mkono na kupasisha azimio hilo.

Kura hiyo ilifuatia juhudi endelevu za Wademokrati katika mabunge yote mawili ili kupunguza mamlaka ya Trump kuhusu hatua za kijeshi zinazohusisha Iran, mpango ambao umeungwa mkono pia na Warepublican katika wiki za hivi karibuni.

Azimio hilo liliwasilishwa na Mwakilishi Gregory Meeks wa New York, Mdemokrati aliyeorodheshwa katika Kamati ya Masuala ya Nje ya Baraza la Wawakilishi.

“Wenzangu wengi kutoka chama cha Republican wanahisi mashinikizo nyumbani wanapoangalia gharama ya chakula, na gharama za mafuta,” amesema Meeks.

Hatua hiyo, bado inahitaji kupasishwa na Baraza la Seneti ya Marekani, lakini haihitaji saini ya rais.

Vyombo vya habari vinasisitiza kwamba hii ni kura ya kwanza ambapo Baraza la Wawakilishi limefanikiwa kupunguza mamlaka ya vita ya Trump kuhusu mzozo wa Iran na hatua za kijeshi za siku zijazo bila idhini ya Kongresi.

Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zilianzisha vita vya kichokozi na bila sababu dhidi ya Iran mnamo Februari 28.

Iran ilijibu kwa kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi yaliyofanikiwa na ya kimkakati dhidi ya shabaha nyeti na za kimkakati za Marekani na Israel katika eneo lote la Asia Magharibi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *