Mali inatoa zawadi ya dola milioni 3.5 kwa taarifa zitakazopelekea kukamatwa kwa Iyad Ag Ghaly, mkuu wa tawi la Al Qaeda katika ukanda wa Sahel; Ghaly pia yuko kwenye orodha ya magaidi wa Marekani na anakabiliwa na hati ya kukamatwa iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu, ICC.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka imetenga zawadi ya kifedha kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa au kuuawa kwa viongozi wa JNIM au FLN. Ghaly, kiongozi wa kundi la JNIM, anatajwa kuwa mtu anayesakwa zaidi katika eneo hilo kutokana na kuongoza kundi kubwa la wanajihadi linalopambana na tawala za kijeshi nchini humo na katika mataifa jirani.

Katika tangazo lililotolewa mnamo Juni 4, 2026, kwenye televisheni ya serikali ORTM, serikali ya mpito ya Mali inatoa zawadi ya kifedha kwa yeyote atakayetoa taarifa zitakazopelekea kukamatwa au kuuawa kwa viongozi wa wanajihadi wa JNIM, wanaohusishwa na Al Qaeda, au washirika wao wa FLN wanaotaka kujitenga. 

Kwa mujibu wa taarifa ya wizara ya usalama, zawadi hiyo ni faranga bilioni mbili za CFA, huku dola milioni 2.5 zikitolewa kwa taarifa zitakazosaidia kumpata naibu wake Amadou Kouffa. Pia zawadi nyingine zimetolewa kwa viongozi wa waasi wa Tuareg. 

Viongozi hao wanaosakwa ni: Iyad Ag Ghaly, Hamadoun Kouffa, Seidane Ag Hitta, wa JNIM au Alghabass Ag Intallah na Bilal Ag Acherif, wa FLA. Zawadi hizi zinaanzia faranga milioni 500 hadi bilioni 2 za CFA.

Mali imekuwa ikikumbwa na machafuko kwa takriban miaka 15, yakihusisha makundi ya wanajihadi, wapiganaji wenye uhusiano na Dola la Kiislamu pamoja na magenge ya kihalifu, huku nchi ikiendelea kuongozwa na serikali ya kijeshi tangu mapinduzi ya 2020.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *