
Kongamano la chama cha PASTEF limefanyika Jumamosi jioni katika vitongoji vya Dakar. Ousmane Sonko alichaguliwa tena kwa kauli moja kuwa kiongozi wa chama, huku uchaguzi wa urais wa 2029 ukikaribia. Chama hakikuamua kuhusu hatima ya mawaziri waliobaki katika serikali mpya, wala ile ya rais Bassirou Diomaye Faye, ambaye anasalia kuwa mwanachama wa heshima licha ya kutengana na mshirika wake wa zamani.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Dakar, Juliette Dubois
Ousmane Sonko alichaguliwa tena kwa kauli moja. Kwa kura 589 kati ya 589, wajumbe wa PASTEF walimchagua kwa muhula wa miaka sita. Ni mwanzilishi wa mradi wa chama tangu kuanzishwa kwake mwaka wa 2014, na ndiye anayepaswa kuuendeleza mwaka wa 2029 kwa ajili ya uchaguzi ujao wa rais.
“Tumekuwa tukijivunia yeye tangu mwanzo hadi leo,” anasema mmoja wa wafuasi wake. “Lengo tulilokuwa nalo mwaka wa 2019, ambalo tulilitekeleza hadi mwaka 2024, ndilo lengo lile lile tutakalotekeleza hadi mwaka 2029, Mungu akipenda, ambalo ni kumweka Rais Ousmane Sonko katika uongozi wa nchi hii,” alisema mfuasi mwingine wa PASTEF.
Lengo liko wazi sasa kwa kuwa kutengana na rais Bassirou Faye kumekamilika na PASTEF imerudi upinzani. “Sasa, PASTEF inajitengenezea njia yake yenyewe kwa Mwongozo wake wa Mapinduzi, bila Rais wa sasa wa Jamhuri,” alibainisha Ibou Daga Ndao, mjumbe kutoka Bakel, mashariki mwa nchi. “Kwa sababu hatuzungumzi lugha moja tena.”
Je, hii ina maana kwamba Bassirou Faye anapaswa kufukuzwa kutoka chama, pamoja na mawaziri wa PASTEF waliobaki katika serikali mpya licha ya wito wa Ousmane Sonko wa kususia? Sio lazima, kulingana na Mbunge Bakary Diedhiou: “Unajua kwamba chama cha PASTEF kilitoa taarifa ikisema kwamba mawaziri hawa wote wa zamani lazima waondoke serikalini, na kwamba yule aliyebaki hakubaki kwa jina la PASTEF, bali kwa jina lake mwenyewe. Kwa hivyo, hii ina maana kwamba watu hawa wamejitenga wenyewe.”
Leo Jumapili alasiri, Ousmane Sonko atalakiwa katika mkutano wa hadhara wa kutawazwa kwake katika ukumbi wa Arenawa de Diamniadio.