Wanajeshi wa Marekani wametekeleza mashambulio nchini Iran, baada ya rais Donald Trump kuishtumu nchi hiyo kwa kuiangusha helikopta ya kivita ya Marekani, iliyokuwa inapaa juu ya angaa katika eneo la mlango wa Bahari ya Hormuz.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kituo cha Kamandi ya jeshi la Marekani limesema, mashambulizi hayo yalilenga kujibu hatua ya Iran isiyokubalika na ya makusudi baada ya kushambulia na kuangusha helikopta yake ya kijeshi.

Mashambulizi ya Marekani yameharibu miundo mbinu ya rada na kulenga bandari za Bandar Abbas, Qeshm na Sirik.

Marubani wawili waliokuwa kwenye helikopta hiyo ya Marekani, waliokolewa bahari, huku rais Donald Trump akisema hawakujeruhiwa na wapo katika halin nzuri ya afya.

Nalo jeshi la ulinzi wa mapinduzi ya Iran, limesema limetumia ndege zake zisizokuwa na rubani kushambulia kambi ya jeshi la Marekani nchini Bahrain na Jordan, baada ya kushambuliwa.

Waziri wa Mambo ya nje wa Iran Abbas Araghchi, amesema Marekani ilichagua kuijaribu nchini yake, na kuongeza kuwa wanajeshi wa Iran watajibu mashambulizi yoyote, iwapo itashambuliwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *