Nchini Kenya, mtu mmoja ameuawa baada ya kupigwa risasi na polisi, wakati wa maandamano yaliyofanyika siku ya Jumanne katika mji wa Nanyuki, baada ya wenyeji kujitokeza kupinga kujengwa kwa kituo cha Karatini cha ugonjwa wa Ebola, utakaowapa hifadhi raia wa Marekani.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Shirika la kutetea haki za binadamu la Vocal Africa, limesema mtu aliyeuawa alipigwa risasi kichwani, wakati maafisa wa usalama walipotumia nguvu kuwakabili waandamanaji.

Wakaazi wa Nanyuki wameapa kuendelea kuandamana, hadi pale kilio chake kitakaposikika na kuondoa kituo hicho cha Ebola kinachonjengwa katika kambi ya jeshi la angani ya Laikipia.

Kenya ambayo haina maambukizi ya Ebola, imesisitiza kuwa kituo hicho kinajengwa na Marekani ili kuwasaidia raia wake watakaokuwa wameambukiziwa ugonjwa huo ambao unaendelea kusambaa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wizara ya afya nchini Kenya, inasema kituo hicho pia kitatumiwa na Wakenya iwapo maambukizi ya Ebola yataripotiwa nchini humo.

Hata hivyo, wenyeji wa Nanyuki wanaishtumu serikali ya Kenya kwa kuhatarisha maisha yao kwa kujenge kituo hicho katika eneo hilo, huku wakisisitiza kuwa hawataruhusu uwepo wake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *