.

Chanzo cha picha, Getty Images

Iliyochapishwa

Muda wa kusoma: Dakika 8

Kaka wa Brazil ndio mwanzo alikuwa ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Fifa 2007 lakini hafla ya kuwazawadia washindi zawadi zao ilizua gumzo lililoishia kuwa ushindani katika historia ya soka.

Lionel Messi na Cristiano Ronaldo walikuwa wamemaliza wa pili na wa tatu mtawalia lakini nguli wa Brazil Pele alimpa mshindi wa pili zawadi ya nafasi ya tatu kwenye Jumba la Opera mjini Zurich.

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) Sepp Blatter alilazimika kuingilia kati tukio hilo na kuwaambia wawili hao kubadilishana tuzo hizo, na walionekana kutoridhithishwa na hatua hilo.

Kwa miaka 10 iliyofuata, Messi au Ronaldo walishinda kila tuzo ya Ballon d’Or na Fifa. Tangu 2007, matuzo 20 kati ya 29 zilizotunukiwa mchezaji bora wa mwaka wa Ulaya iliemuendea mmoja wao.

Huku kila mmoja wao akikaribia kufunga mabao 2,000, kushinda mataji 85 ya klabu na nchi na tuzo nyingi za watu binafsi, Messi na Ronaldo daima watakumbukwa kama wachezaji wawili waliotunikiwa zaidi katika historia.

Ni mchuano ambao umefafanua miongo miwili iliyopita ya kandanda, vilabu, nchi na mashindano yaliyopita ili kurekebisha jinsi mchezo ulivyochezwa, kutumiwa na kujadiliwa kote ulimwenguni.

“Wachezaji wawili kama wao, wanaoshindana katika kiwango hicho kwa miaka mingi, wakipigania Ballon d’Or na kufunga mabao mengi kiasi hicho… sidhani kama tutaiona tena,” mshindi wa Kombe la Dunia la Argentina Angel di Maria, ambaye alicheza na wote wawili, anasema katika kipindi kipya cha BBC Sport Rivals: Messi v Ronaldo.

Wakisukumwa naari ya kushinda mataji, na hamu ya kudumu ya kuwa mchezaji bora zaidi, wawili hao – ambao huenda wanacheza mechi zao za mwisho za Kombe la Dunia msimu huu wa joto – ushindani wao umefikia kiwango kipya.

Ni ushindani ambao ni zaidi ya mjadala wa mchezaji ‘bora wa wakati wote’ ambao walichochea.

“Wote wawili walibadilisha soka,” anasema Di Maria.

.

Chanzo cha picha, Getty Images

Ukimuuliza mtu yeyote ni mchezaji gani bora zaidi kati ya Messi na Ronaldo huenda usipate jibu kutokana na mjadala utakaoibuka.

“Bila shaka ni Ronaldo,” mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United Rio Ferdinand anasema.

“Messi ndiye bora zaidi hana mshindani,” anasisitiza mchezaji na meneja wa zamani wa Barcelona Xavi.

Ronaldo amekuwa na maoni yake siku za nyuma, akisema mwaka 2012: “Huwezi kulinganisha Ferrari na Porsche. Ni injini tofauti. Baadhi ya watu wanasema mimi ni bora zaidi, wengine wanasema yeye. Wataamua nani bora kwa sasa na nadhani ni mimi.”

Takwimu zinasema nini? Ikiwa itaamuliwa kwa mabao au mataji ya Ligi ya Mabingwa, Ronaldo anaongoza. Ikiwa ni Ballons d’Or au jumla ya mataji, Messi anaifunika.

Kwa baadhi ya watu, Ronaldo alitangulia mbele alipoisaidia Ureno kubeba Ubingwa wa Uropa mwaka wa 2016, lakini Messi ameiongoza Argentina kushinda mataji mawili ya Copa America na Kombe la Dunia.

“Kwangu mimi, Messi ndiye mchezaji bora zaidi katika historia na Cristiano ndiye mfungaji bora zaidi katika historia,” anasema mtaalamu wa soka wa Uhispania Guillem Balague, ambaye ameandika wasifu wa wachezaji wote wawili.

Naye Deco, ambaye alicheza na Ronaldo katika timu ya taifa ya Ureno na Messi kwa katika timu ya taifa ya Barcelona, ​​anasema: “Wote wawili ni maalum. Ni tofauti kabisa na wengine. Sio kawaida kuwa katika kiwango hiki miaka yote.

“Kila mwaka, kuna wachezaji wengi waliofanya vyema kwa miaka kadhaa, lakini kishikilia nafasi hiyo kwa takriban miaka 20 sio jambo la kawaida.”

Uzuri wa mjadala wa mjadala wa mchezaji bora wa muda wote (GOAT) ni kwamba huenda usifikie mwisho – na sio lazima uhitimishwe.

“Wamekuja kuthaminiana kama wachezaji nyota wa kandanda kwa miaka 20 iliyopita,” anasema Jonathan Clegg, mwandishi mwenza wa kitabu cha Ronaldo na Messi.

Wawili hao wanaonekana na wengi kama washindani tofauti kabisa.

Mchezaji mwenye chenga dhidi ya anayetumia mabavu. Mwenye haya dhidi ya mwenye kiburi. Barcelona ya Pep Guardiola dhidi ya Real Madrid ya Jose Mourinho. Adidas dhidi ya Nike

Lakini, wakati wa masimulizi ya ushindani wao bila shaka yalijengwa kwenye tofauti zao, mfanano kati ya wawili hao ulikuwa wa kushangaza – hata tangu umri mdogo.

Wachezaji wote wawili walilelewa katika mazingira duni. Wote wawili waliondoka nyumbani wakiwa na umri mdogo ili kutimiza ndoto zao – Messi kwenda Barcelona kutoka Argentina akiwa na umri wa miaka 13 na Ronaldo hadi Lisbon kutoka Madeira wenye umri wa miaka 12 – na wote walitatizika na ugonjwa wa nyumbani baada ya kuacha familia zao.

Mwandishi wa Jarida la Wall Street Joshua Robinson, mwandishi mwenza wa kitabu cha Messi Ronaldo, alisema: “Messi na Ronaldo siku zote wanaonyeshwa kuwa tofauti sana lakini mambo ambayo yaliwazua katika utoto wao yalifanana sana.

“Wote wawili huenda mahali panaposema ‘tutachukua kipaji chako na kukufanya mkubwa zaidi’. Ahadi hiyo inapendeza lakini ni kamari kubwa. Wakati huo wa kujitolea kabisa ndipo wanapogundua kuwa haya si mambo ya mtoto tena. ‘Ikiwa nitakuwa mkuu zaidi wa wakati wote, hapa ndipo inapoanzia.’

Lakini jambo kubwa lililowakutanisha wawili hao ni hamu yao isiyotikisika ya kutaka kufanikiwa kwani haraka walijijengea sifa ya kuwa vijana wenye vipaji vya hali ya juu.

“Tayari unaweza kuona kitu tofauti na Messi,” alisema Xavi. “Sio ubora tu, bali pia kasi aliyotumia kufanya mambo. Kulikuwa na uchokozi katika ushambuliaji ambao sikuwahi kuuona hapo awali.

“Cristiano hata alimpa msukumo wa ziada kuwa mchezaji bora.”

Wakati huohuo huko Uingereza, Ronaldo kijana alikuwa akisajiliwa na Manchester United kutoka Sporting.

“Sijawahi kukutana na mchezaji mchanga ambaye anajiamini sana kujua anachotaka,” alisema Rene Meulensteen, ambaye alikuwa sehemu ya timu ya nyuma ya klabu wakati huo. “Wakati alipokuja Man United ilikuwa ni hatua ya kimantiki ya kile alitaka kuwa – mchezaji bora zaidi duniani.

“Cristiano alikuwa mwanafunzi wa kasi. Nilitaka kumgeuza kutoka kwa mtu ambaye angeweza kufunga bao hadi mfungaji mabao. Nilitengeneza video ya dakika tatu ambayo ilionyesha tu akifunga mabao na pia nafasi ambazo hakufunga. Alikumbatia kila kitu.”

Kusonga mbele hadi 2008 na nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa. Manchester United v Barcelona. Ronaldo v Messi kwa mara ya kwanza.

“Unaweza kuona tayari Messi alikuwa bora kwenye La Liga na Cristiano alikuwa bora zaidi kwenye Ligi Kuu,” mwandishi wa habari wa soka wa Uhispania Guillem Balague alisema. “Kuwaona watoto hao wawili uwanjani pamoja ilikuwa ishara ya kitu kinakuja.”

Manchester United waliendelea kushinda taji hilo, Ronaldo akanyanyua Ballon d’Or na ushindani wa miaka mingi ulikuwa umeanza.

“Bila shaka kucheza katika ligi moja kulibadilisha kila kitu,” anasema Txiki Begiristain, mkurugenzi wa soka wa Barcelona kati ya 2003 na 2010.

Uhamisho wa kuvunja rekodi wa pauni milioni 80 wa Ronaldo kwenda Real Madrid mwaka 2009 uliwafanya wawili hao kujipatta katikati ya mojawapo wa ushindani wa klabu ya soka – Barcelona v Real Madrid.

Hadi wakati Ronaldo alipohamia Juventus mnamo 2018, wawili hao walikuwa wameshinda tuzo ya Ballons d’Or tano kila mmoja. Katika misimu tisa wawili hao wakiwa pamoja nchini Uhispania, Ronaldo alikuwa amefunga mabao 450 katika mechi 438 aliyoichezea Real. Messi, 471 katika mechi 476 ya Barca.

Lakini ushindani ulikuwa zaidi ya ufungaji mabao. Kufikia sasa, ilikuwa ya kibinafsi – na ukuaji wa mitandao ya kijamii ulimaanisha ulimwengu ulikuwa ukiwafuatilia.

“Kwa Cristiano alikuwa Lionel Messi na kwa Lionel Messi alikuwa Cristiano. ‘Nahitaji kumshinda kijana huyu’,” alisema Begiristain.

“Ushindani wa Mourinho – Guardiola ulikuwa kama kioo cha ushindani wa Ronaldo – Messi. Na, kama wachezaji, walijua kwamba mabao ya kushinda mchezo yalikuwa njia yao ya kuwa bingwa,” aliongeza mwandishi wa soka wa Uhispania Sid Lowe.

“Tuliweza kuitazama yote kwenye simu zetu. Na kwa upande mwingine, ushindani wa kimataifa wa Messi – Ronaldo sasa ulikuwa wa hali ya juu, nje ya chati. Kila kitu walichofanya ni lazima kuona.

“Ilikuwa midomoni mwa kila mtu kwenye vyumbo vya wanahabari, magazeti na maoni kwenye mitandao ya kijamii, Cristiano na Leo walikuwa wamedhamiria kuzidiana uwanjani. Vita vyao vya kibinafsi vya kuwania ukuu viliashiriwa na vita vya kuwania taji kati ya vilabu vinavyoendelea.”

Na ilikuwa mchuano hasa. Messi na Barcelona bila shaka walishinda tuzo za La Liga, lakini Ligi ya Mabingwa ilitawaliwa na Real Madrid na Ronaldo.

Mwaka wa 2012, Ronaldo aliiwezesha Real kushinda taji lao la kwanza la La Liga katika kipindi cha miaka minne lakini ni Messi ambaye alijinyakulia tuzo yake ya nne mfululizo ya Ballon d’Or – jambo lililomchukiza sana mpinzani wake. Aliendelea na kushinda nne kati ya tano zilizofuata.

“Kuna chuki ya kweli ambayo inaanza kukua,” anasema Robinson. “Hawakukubaliana kiasi hicho, walichukia kulinganishwa.

“Hawangeweza kuvumilia kama wangekuwa bora zaidi wakati wote, kunaweza kuwa na mwingine katika zama zao, kwenye ligi yao ya soka.”

Deco anaongeza: “Sidhani kama kuna kitu kama kile kilichotokea kwa Messi na Ronaldo kwa wakati huu kwa sababu wakati huo huo vilabu viwili, Barcelona na Madrid, vilikuwa katika kiwango sawa na kupigania mataji makubwa.”

Wakati Messi alipoifungia Barcelona bao la ushindi dakika ya 92 wakiwa Real Madrid mwaka 2017, alivua jezi yake na kuinua umati wa watu.

“Katika simulizi maarufu, Cristiano alikuwa diva na Messi alikuwa mtumishi mnyenyekevu wa Barcelona, ​​lakini hii ilikuwa wakati wa Messi kujisisitiza juu ya ushindani, akisema labda kwa mara ya kwanza katika maisha yake ‘niangalie’,” anasema Robinson.

Miezi michache tu baadaye, Ronaldo aliiga sherehe hiyo alipofunga katika Kombe la Super Cup la Uhispania huko Barcelona.

Balague aliongeza: “Ikiwa ulihitaji uthibitisho wa ni kiasi gani kilimaanisha kupigana, hizo ndizo picha.”

Messi na Ronaldo

Chanzo cha picha, Getty Images

Ushindani wa Messi dhidi ya Ronaldo nchini Uhispania huenda uliisha wakati Ronaldo alijiunga na Juventus mnamo 2018 – lakini mjadala wa kimataifa, unaoendelea haukupotea.

Ronaldo alirejea Manchester United kabla ya kuhamia klabu yake ya sasa ya Al-Nassr ya Saudi Arabia, huku Messi akihamia Paris St-Germain, kabla ya kusajiliwa na Inter Miami inayoshiriki Ligi Kuu ya Soka ya Marekani – ambako anakipiga mpaka sasa.

Baada ya kuona athari zao nchini Uhispania, kwa mara ya kwanza uhamisho wa wachezaji hao ulikuwa na msukumo wa kibiashara kama walivyokuwa kwa sababu za soka.

“Brand Beckham alifungua mlango kwa kile kilichowezekana na wawili hawa wamepiga mlango kutoka kwenye bawaba zake,” Rob Pilgrim, mkuu wa michezo wa Meta kwa Ulaya, Mashariki ya Kati na Afrika alisema.

Mtaalamu wa soka wa Italia Mina Rzouki, aliongeza: “Hununui ubora wa michezo, unanunua uchumi wa mtu mmoja.”

Nambari ni za angani na ushindani uliendelea.

Mnamo 2018, Ronaldo alijiunga na Juventus na kuuza jezi 520,000 ndani ya masaa 24 ya kwanza. Mnamo 2021, Messi anahamia Paris na kubadilisha jezi 150,000 ndani ya dakika saba tu.

Manchester United inamkaribisha Ronaldo tena mwaka wa 2021, na jumla ya mauzo ya United ya jezi yake (£187m) ni karibu mara mbili ya yale ya Messi akiwa PSG.

Kwenye mtandao wa Instagram, Ronaldo ana wafuasi karibu milioni 700, Messi ana milioni 500. Picha inayopendwa zaidi katika historia ya jukwaa hilo ni Muagentina huyo akinyanyua kombe la Kombe la Dunia, na kujikusanyia zaidi ya likes milioni 75.

Kifedha, Ronaldo anaibuka kidedea – kulingana na vyanzo rasmi hata hivyo. Mreno huyo ameongoza orodha ya Forbes Money kama mwanariadha anayelipwa zaidi duniani kwa mara ya nne mfululizo, akiwa na mapato ya jumla ya $300m (£223m). Messi ni wa tatu kwenye orodha hiyo akiwa na $140m (£104m).

Ushindani kati ya wawili hao umehanikiza mpaka katika ulingo wa biashara. Messi akiwa na Adidas na Ronaldo akiwa na Nike.

“Wamekuwa chapa kubwa za kimataifa na kinachowashangaza ni kwamba hawana la kusema chochote isipokuwa wanasoka mkubwa zaidi duniani,” alisema Robinson.

Chapa ulimwenguni kote zilituma pesa nyingi zisizo na kifani ili kuwapata nyota hao kwenye bango.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *