
Jeshi la Marekani limetangaza kufanya mfululizo mwingine wa mashambulizi dhidi ya Iran katika taarifa iliyotolewa kwenye mtandao wa kjamii wa X.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Vikosi vya Marekani “vimefanya mashambulizi mapya ya kujihami dhidi ya malengo mengi nchini Iran, kama ilivyoelekezwa na kamanda mkuu,” imeandika CENTCOM, kamandi ya jeshi la Marekani kwa Mashariki ya Kati.
“Vikosi vya CENTCOM vimeanzisha mashambulizi dhidi ya vituo vya ufuatiliaji wa kijeshi vya Iran, mifumo ya mawasiliano, na maeneo ya ulinzi wa anga kote nchini,” taarifa hiyo imeongeza.